Mwanamume mmoja nchini Uchina amehukumiwa kifungo gerezani kwa makosa ya kushtua kuku wa jirani yake hadi wakaaga dunia.
Mwanamume huyo kwa
jina Gu anaripotiwa kuingia kisiri katika shamba la jirani yake kabla ya
kushtua maelfu ya kuku na kuwaaacha wamefariki.
Mahakama ya Hengyang
iliambiwa kuwa Gu alitumia tochi kuwatishia ndege hao 1100 na kuwafanya kuuana
- hii ikiwa njama yake ya kulipiza kisasi dhidi ya jirani yake
inaripotiwa kuwa
mwangaza huo ulifanya kuku hao waliokuwa wamshtuka kukimbilia kwenye kona na
kuuana kwa kukanyagana.
Gu alikuwa akilipiza
kisasi katika mzozo wao ulioanza Aprili 2022 jirani yake alipokata miti yake
bila ruhusa japo alipigwa kifungo cha miezi sita gerezani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.