Polisi mjini Kisumu wanachunguza kisa ambapo afisa mmoja wa polisi alirushua vitoa machozi katika maeneo kadhaa ya burudani mkesha mjini humo usiku wa kuamkia Jumatatu
Kwa mujibu wa ripoti
ya polisi, kisa hicho kilitokea mwendo wa saa tisa asubuhi, polisi huyo
akimshuku mpenzi wake kutoka na mwanamume mwengine.
Kisa cha kwanza
kilitokea katika hoteli moja ambapo afisa huyo alishuku kuwa mpenzi wake alikuwa
amekodi chumba na mwanamume mwengine.
Baada ya ugomvi na
mlinzi ambaye alimzuia kuingia hotelini humo, inaripotiwa kuwa afisa huyo wa
polisi alirusha kitoza machozi hotelini humo
Polisi huyo baadaye
aliondoka eneo hilo kwa kutumia pikipiki baada ya juhudi za kuingia hotelini
humo kukosa kufua dafu.
Mshukiwa alielekea
eneo la Nyamasaria kwenye barabara kuu ya Kisumu kuelekea Nairobi na kurusha
kitoza machozi katika eneo la burudani ambako wananchi walikuwa wanaburudika.
Alivamiwa na kukamatwa
na umati akitambuliwa kuwa afisa wa polisi.
Alipata majeraha
mabaya na kukimbiza katika Hospitali ta Mafunzo na Rufaa ya Jaramogi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.