Zaidi ya wanandoa 800 walifika kanisani Jumapili ya Pasaka katika moja ya sherehe kubwa ya harusi nchini Afrika Kusini tangu mlipuko wa janga la Covid 19.
Kanisa
la International Pentecost Holiness linabariki ndoa za wanaume wenye wake
wengi, ambazo ni za kawaida katika baadhi ya jamii za Kiafrika, na kanisa hilo
linasema kuwa zimeidhinishwa na Biblia.
Misa
ya wanandoa wengi hufanyika mara tatu kwa mwaka, siku ya Pasaka, mwezi Disemba
na wakati wa maadhimisho ya mwezi Septemba ya kuanzishwa kwa kanisa hilo mwaka
1962.
Lebogile
Mamatela, mwenye umri wa miaka 38, ambaye ni mfanyakazi wa serikali ambaye
amekuwa mke wa pili kwa baba wa binti yake jana Jumapili, aliiambia Reuters
baada ya hafla hiyo: Ni siku isiyo ya kawaida, nina furaha sana. Ninathamini
sana wakati huu kwa kuwa miongoni mwa familia ya Mahluku. Ni hisia nzuri.”
Mume
wake, Roto Mahluku mwenye umri wa miaka 40, alijiunga na kanisa hilo mwaka 1993
na alimuoa mke wake wa kwanza, Ditopa Mahluku miaka 16 iliyopita. Wana watoto
watatu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.