Mhubiri ambaye alifariki mwaka 2021 jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini na mwili wake kuhifadhiwa na kuombewa akitarajiwa kufufuka hatimaye amezikwa.
Mwili wa pasta wa Gauteng -
Siva Moodley - umekuwa katika makafani ya Johannesburg tangu Agosti 15, 2021
alipokumbana na mauti.Mwanzilishi huyo wa kanisa la The Miracle Centre lililo
kaskazini mwa Johannesburg aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 53 baada ya kuwa
mgonjwa.
Kwa mujibu wa ripoti ya
awali ya jarida la OIL, familia ya Mooley na washirika wake wamekuwa wakizuru
makafani hayo kusali ili afufuke.
Licha ya haya, meneja wa
makafani hayo Martin du Toit aliwasilisha ombi katika mahakama ya Johannesburg
akitaka ruhusa ili auzike au kuuchoma mwili wa Moodley.
Tangu kufa kwake, inaarifiwa
ibada zimekuwa zikiendelea katika kanisa lake, zikiendeshwa na mke wake Jessie,
na wanawe wawili David na Kathryn Jade.
Ibada hizi hupeperushwa moja kwa moja kwenye
mitandao ya kijamii. Hata hivyo inaarifiwa kuwa kanisa halijakiri kufariki kwa
mhubiri huyo.
Kutokana na hilo, inadaiwa
halijatangaza kifo chake kwenye mitandao ya kijamii wala kuwaambia washirika
aliko pasta wao.
Pia imearifiwa kuwa akaunti
za Moodley kwenye mitandao ya kijamii - hususan Facebook na Twitter - bado
zinafaya kazi na jumbe kuanikwa hapo kila siku kanakwamba zinatoka kwake.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.