Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amewaambia raia kwamba haki zao za kuandamana "hazimpi yeyote haki ya kunyanyasa, kutisha au kumtishia mtu yeyote".
Pia ameonya dhidi ya uharibifu wa mali au kuwadhuru watu
wengine.
Hii inakuja huku maandamano yaliyoandaliwa na chama kikuu cha
upinzani cha- Economic Freedom Fighters (EFF) yakifanyika kote nchini humo.
Maandamano hayo yaliyopewa mada ya -usimamishwaji wa shughuliza
kitaifa, waandamanaji wanamtolea wito Rais Cyril Ramaphosa kujiuzulu huku
wakimshutumu kwa ufisadi na kushindwa kushughulikia mzozo wa nishati.
Hadi sasa polisi wa Afrika Kusini wamewakamata watu 87 kuhusiana
na maandamano.
Serikali pia imewaweka
zaidi ya wanajeshi 3,000 kusaidia kulinda miundo mbinu.
"Kama vile taifa lina jukumu la kuuunga mkono haki ya
maandamano ya amani, lina wajibu pia wa kuzuia jaribio lolote la kukiuka haki
yoyote ya kikatiba.’’ Rais alisema katika taarifa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.