ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 20, 2023

MWANAMKE MNIGERIA AFARIKI AKIFANYIWA UPASUAJI WA KUONGEZA MAKALIO,


Simanzi imeghubika Nigeria, kufuatia kifo cha mrembo mwenye umri wa miaka 20, ambaye anasemekana alifariki akifanyiwa upasuaji wa kuongeza makalio.

Kulingana na swahiba wa marehemu, Destiny Jojo, alikwenda katika hospitali ya urembo jijini Lagos kwa upasuaji huo na alitarajiwa kuruhusiwa kwenda nyumbani baada ya siku nne

.Hata hivyo, alikumbana na matatizo ya kupumua kisha alikimbizwa katika hospitali ya mtalaam ambapo aliaga dunia.

 Hospitali yapinga

Kufuatia taarifa za kifo cha Destiny kuibuka mitandaoni mnamo Jumatano, Machi 15, hospitali ambako anadaiwa kufanyiwa upasuaji huo ilikashifiwa vikali na wanamtandao kwa kile walitaja kama utepetevu kwa upande wa madaktari.

Wanamtandao waliishutumu vikali hospitali na kuitaka serikali ya Nigeria kuifunga kabisa ili kuzuia vifo zaidi.

Hata hivyo, hospitali hiyo ya Cynosure Aesthetic, imevunja ukimya wake ikijaribu kuzima habari potofu ambazo zilikuwa zikienezwa kuhusu kifo cha Destiny.Kulingana na hospitali hiyo, uchunguzi wa CT ulifanyiwa marehemu alipofika katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU "na matokeo yalionyesha hakukuwa na shida ya mapafu.

Hospitali hiyo pia ilikanusha madai kuwa mrembo huyo alifariki katika kituo chao, na kufichua kwamba aliaga dunia katika hospitali ya watalaam ya ICU alikopewa rufaa

.Wakati huo huo, mwanamtandao kwenye Twitter alidai kuwa Destiny sio mti wa kwanza kufariki katika hospitali hiyo

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.