ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 21, 2023

NACHINGWEA TAJIRI ILA WANANCHI WAKE WAVIVU

 

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo mwenyewe tishet ya kijani akiwa katibu tawala wa wilaya hiyo Omary Said Mwanga walipofanya ziara kwenye moja ya mgodi wa madini unaopatikana katika wilaya hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo mwenyewe tishet ya kijani akiwa viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo walipofanya ziara kwenye moja ya mgodi wa madini unaopatikana katika wilaya hiyo


Na Fredy Mgunda,. Nachingwea



UTAJIRI wa madini na Kilimo katika wilaya ya Nachingwea kunaifanya wilaya hiyo kuwa moja ya wilaya ambayo tajiri baada ya miaka mitano.

Akizungumza wakati wa ziara ya kijiji kwa kijiji yenye kauli mbiu isemayo ulipo nipo toa kero yako sema kweli, mkuu wa wilaya hiyo Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa wilaya ya Nachingwea imebarikiwa utajili wa kila aina hivyo ni juhudi binafsi zinatakiwa ziongezwe kwa wananchi.

Moyo alisema kuwa wilaya ya Nachingwea ina aina zote za madini ambayo yanatakiwa sokoni hivyo anawakaribisha wawekezaji kuwekeza kwenye sekta ya madini na Kilimo.

Alisema kuwa maono ni kuhakikisha wilaya hiyo inapata wawekezaji wengi kwenye kila sekta ili kuzitumia fursa za kiuchumi zilizopo wilaya humo kama ambavyo malengo ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kuvutia wawekezaji.

Aidha Moyo aliwataka wananchi wa Nachingwea kujituma kulima mazao mchanganyiko ili kuondokana na tatizo la njaa ambalo limewakumba mara kwa mara.

Moyo alisema kuwa wananchi wa wilaya hiyo wavivu kujishughulisha na shughuli za kimaendeleo.

Alisema kuwa wilaya ya Nachingwea imebarikiwa kuwa na ardhi yenye rutuba ambayo haitumiwi vilivyo kuzalisha mazao ya chakula na biashara na kupekea wananchi hao kila mara kuomba chakula cha msaada kwa serikali.

Moyo alisema kuwa Wananchi hawajishughulishi na kilimo badala yake wanategemea kuomba omba omba misaada wakati wananguvu za kutosha kufanya kazi za kilimo.

"Mimi sitaki kusikia wananchi wanalalamika kuhusu njaa wakati ardhi inarutuba kuliko hata baadhi ya maeneo mengi ya wilaya ya Iringa ambako huwezi kusikia wanaomba msaada wa chakula,sasa tutabanana hadi mtaacha uvivu" alisema Moyo

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.