18 Februari 2023:
Watoto wenye ulemavu na wasiojiweza wa Kituo cha Hopes kilichopo Miono Chalinze mkoani Pwani, wamefutwa machozi na Taasisi ya Tete (Tete Foundation) kwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya Reliance na Benki ya DTB Tawi la Dodoma kwa kupewa msaada wa vitu vilivyokuwa changamoto kwao.
Tete Foundation na wadau wake walifika kwenye kituo hicho na kuwapatia watoto hao msaada wa vitu mbalimbali ambavyo awali vilikuwa changamoto kwao.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Tete Foundation, Suzana Senso alisema kabla ya kufikiria kupeleka msaada kwenye kituo hicho walifanya utafiti na kugundua vituo vingi kama hivyo vinavyohitaji msaada lakini kituo hicho kinahitaji msaada zaidi.
Suzana amesema baada ya kubaini changamoto hiyo aliwasiliana na Kampuni ya Bima ya Reliance Tanzania Limited ambayo kwa uzalendo wake nao hawakusita kukubali ombi la kuwachangia msaada huo.
Suzana aliendelea kusema kuwa wengine waliomchangia ni Benki ya DTB Tawi la Dodoma ambao wote kwa pamoja aliwashukuru sana. Aliendelea kusema Suzana;
“Tunamshukuru Mungu siku ya leo ambayo imekuwa ni siku ya kipekee tukiwa tunakamilisha kampeni yetu iliyoitwa ‘Tunaamini Katika wewe’ wewe huku maeneo ya Miono Bagamoyo Chalinze mkoa wa Pwani tuliyoianzisha tarehe 9 Januari mwaka huu.
“Tunaposema tunaamini katika wewe ‘buku’ yako moja inakwenda kumgusa mtoto mmoja anayeishi katika mazingira magumu kwa kumnunulia peni au penseli.
“Tumekuwa na hii kampeni kwa karibia mwezi mmoja na nusu na leo ndiyo tumefikia kilele huku Miono. Lakini kikubwa zaidi tumeweza kuwapatia watoto hawa msaada mkubwa zaidi ya tulivyotarajia.
“Tunawashukuru wote waliojitoa kwa moyo wao wa uzalendo lakini shukrani za kipekee ziwaendee Reliance Isurance Tanzania Limited kupitia Benki ya DTB waliotuunganisha nao na kutuwezesha kutimiza lengo letu.
Pia tunawashukuru sana wale wote waliokuwa wakichanga zile elfu moja moja zao kupitia zile lipa namba zetu tulizokuwa tumeziweka kwenye mitandao ya kijamii.
“Nipende kutumia nafasi hii kumshukuru Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Reliance Insurance Tanzania Limited, Madam Rukia Goronga na msafara wake kwa kuonesha kujali zaidi na kutumia muda wao kuhudhuria tukio hili pia Meneja wa DTB Benki mkoa wa Dodoma ambaye ametumwa mwakilishi wake baada ya kupatwa na dharura Mungu ambariki sana.
“Nachukua nafasi hii kuwasihi wananchi wengine popote walipo wawakumbuke watoto kama hawa kwa maana tulivyotembea sehemu mbalimbali maeneo haya tulikuta watoto wa wakiwa na mahitaji mbalimbali na wengine kutumia daftari moja kuandikia masomo yote.
“Naibu Mkurugenzi wa Reliance Insurance, Rukia Goronga akizungumza kwenye hafla hiyo baada ya kujionea yaliyokuwa yakiendelea aliipongeza kampeni hiyo na kuahidi kampuni yake kuiunga mkono kwa siku zijazo.
“Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Miono na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Mheshimiwa Juma Ramadhani ameipongeza Tete Foundation kwa kuichagua kata yake kutoa msaada huo na kuimbea kwa Mungu taasisi hiyo izidi kustawi na kuzidi kusaidia kata hiyo na sehemu nyingine.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.