Rais wa zamani wa Zimbabwe hayati Robert Mugabe (kushoto) na mwanawe Junior.
Mwanawe rais wa zamani wa Zimbabwe hayati Robert Mugabe - Robert Tinotenda Mugabe Junior - amekamatwa na maafisa wa polisi nchini humo kwa tuhuma za uharibifu wa mali.
Kwa mujibu wa polisi, Mugabe Junior mwenye umri wa miaka 31 aliharibu magari na mali zingine katika sherehe moja katika jiji kuu la Harare wikendi iliyokamilika.
Taarifa kutoka kwa ofisi ya Kamishna Jenerali wa Polisi imesema kuwa Mugabe Junior alikamatwa baada ya rafiki yake kwa jina Sindiso Nkatazo kupiga ripoti.
Polisi wanasema kuwa mali zilizoharibiwa ni za thamani ya takriban shilingi milioni 1.5 pesa za Kenya.
Shirika la habari la ZimLive limepakia video mtandaoni Mugabe Junior ambaye ni mbunifu wa mitindo ya nguo akipelekwa mahakamani. Junior ni mtoto wa pili wa Mugabe ambaye aliondolewa kwa nguvu mamlakani mwaka 2019 kabla ya kufariki 2021.
Alikuwa ametaliwa nchi hiyo kwa miaka 37.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.