ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, February 21, 2023

ALIYEBAKA, KUMUUA MKE WA MWENYEKITI AKAMATWA.


NA TITUS MWOMBEKI, 

JESHI la polisi mkoa wa kagera limefanikiwa kumkamata Paschal Kaigwa Marisela (21) mkazi wa kata Kishongo alhamashauri ya Bukoba anayetuhumiwa kufanya mauaji ya aliyekuwa kuwa mke wa mwenyekiti wa mtaa wa National Housing kata Rwamishenye manispaa ya Bukoba Hadija Ismail (29) aliyeuwawa kwa kubakwa na  kupigwa na kitu butu Februari 13 mwaka huu. 


Akithibitisha kukamatwa kwa kijana huyo mbele ya waandishi waandishi wa habari leo kamanda mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa kagera William Mwampaghale-ACP  amesema mtuhumiwa huyo alitoroka na kwenda kujificha vichakani na  Februari 19 mwaka huu alitoka mafichoni baada ya njaa kali ndipo alipoamua kwenda kutafuta msaada wa chakula nyumbani kwa Shangazi yake mtaa wa Kashai Katatorwansi manispaa ya Bukoba. 


"Aliwakuta watoto wa Shangazi yake ambao wanamfahamu na baada ya kumuona ndipo walipiga kilele majirani wakafika na kumkamata kwa kuwa tayari tukio alilofanya lilikuwa limeshatangwazwa na vyombo vya habari na Jeshi la polisi mkoa wa Kagera lilishatoa wito kwa wananchi kutoa taarifa pale mtuhumiwa huyo atakapoonekana kwenye maeneo yao" Alisema ACP Mwampaghale. 


Aidha Jeshi la polisi mkoa wa kagera linawashukuru wananchi kwa ushirikiano walioutoa kwa jeshi la polisi huku akitoa wito kwa wananchi hao kuendelea kutoa ushirikaiano kwa jeshi la polisi ili kutokomeza vitendo vya uhalifu ili  waweze kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.