Rais William Ruto amehudhuria mkutano wa pili na Mawaziri wa Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi. Rais William Ruto akiwa kwenye mkutano na Mawaziri wa Uhuru katika Ikulu.
Ruto aliandaa mkutano huo siku ya Jumatatu, Oktoba 3, na Mawaziri hao wanaoondoka kabla ya kikosi kipya cha Mawaziri wake kupigwa msasa wiki ijayo.
Kwenye picha iliyoonekana waliohudhuria kikao chake ni pamoja na Waziri wa Elimu George Magoha, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, Waziri wa Kilimo Peter Munya, Waziri wa Fedha Ukur Yatani, Waziri wa Utalii Najib Balala na Waziri wa Michezo Amina Mohamed, miongoni mwa wengineo.
Wiki Hii Bado haijabainika ni kwa nini Rais aliitisha kikao hicho, huku kikijiri siku chache baada ya kuzindua Baraza lake jipya la Mawaziri.
Ruto alitanagza Mawaziri wake wapya na na kuunda nafasi ya Waziri mkuu, iliyokabidhiwa Musalia Mudavadi.
Ruto alimteua Kithure Kindiki kuwa Waziri wa Usalama wa Nadani, Njuguna Ndungu kuwa Waziri wa Fedha, Aisha Jumwa (Waziri wa Utumishi wa Umma na Jinsia), Aden Duale (Ulinzi), Wahome (Waziri wa Maji), na Alfred Mutua Waziri wa Masuala ya Kigeni.
Aliyekuwa Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi aliteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu, huku Moses Kuria akiteuliwa kuwa Waziri wa Biashara na Viwanda.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.