Taifa Leo
Gazeti hili linaripotia ziara ya Rais Willim Ruto katika ngome ya mpinzani wake mkuu kisiasa Raila Odinga.
Katika njia ya kuthibitishia taifa kuwa eneo hilo halitabaguliwa kimaendeleo, Rais alianza kumwaga minofu akiahidi kutekeleza miradi ya maendeleo ili kuimarisha maisha ya wakazi. Ilikuwa mara ya kwanza kwa Ruto kutembelea eneo hilo tangu uchaguzi mkuu wa Agosti 9, na haikutarajiwa atatua huko haraka na kuahidi miradi mikubwa ya maendeleo.
Akitoa hotuba yake baada ya kuhudhuria ibada katika kanisa la AIC mjini Homa Bay, Rais aliahidi kurejea katika kaunti hiyo mwezi ujao kuzindua mradi wa ujenzi wa nyumba 400 katika awamu ya kwanza inayolenga nyumba 5000 za bei nafuu.
Rais vile vile alifichua mipango yake ya kufufua miradi iliyokwama katika eneo hilo ikiwemo ujenzi wa barabara muhimu ili kipiga jeki uchumi wa Homa Bay na Nyanza kwa jumla.
The Star
Gazeti hili linaripotia kwamba maafisa wa upelelezi wanachunguza kisa cha daktari mmoja aliyejiuwa baada ya kunywa pombe yenye sumu.
Mwili wa daktari Esther Waceke Munyua ulipatikana nyumbani kwake mtaani Langata. Kando ya mwili wake kulikuwa na mikebe tupu ya pombe, dawa na barua iliyosoma 'msongo wa mawazo upo' Polisi wanasema Waceke ambaye alikuwa anahusumu katika Hospitali ya St Marys, alikuwa pekee yake wakati wa tukio hilo la Septemba 28.
Inaripotiwa pia aliwahi kuokolewa tena kwa jaribio lingine la kujitoa uhai.
The Standard
Gazeti hili linaripoti kuwa jamaa anayedai kuwa mwanawe marehemu Mwai Kibaki amesema kuwa yuko tayari kufanyiwa DNA kuthibitisha rais wa zamani ni baba yake.
Jacob Ocholla Mwai kupitia wakili wake Morara Omoke alimwambia Jaji wa Mahakama ya Milimani, Maureen Odero kuwa huenda mchakato huo utalazimu mwili wa Kibaki kufukuliwa.
Gachagua Asema Kibaki alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 90 mnamo Aprili, na kuzikwa nyumbani kwake katika eneobunge la Othaya.
Daily Nation
Katika chapisho hili, limeangazia hatma ya mayatima wa Raila Odinga baada ya kupoteza urais.
Wanasiasa wengi walioagizwa kukatiza azma yao na kuwapisha wengine ndiyo walipata pigo kubwa baada ya Raila kupoteza kwa Ruto.
Miongoni mwa wale walioathirika sana ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jubilee Raphael Tuju, aliyekuwa waziri wa ulinzi Eugene Wamalwa, Peter Munya, Wycliffe Oparanya na John Mbadi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.