ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 23, 2022

WAPORA UNGA BAADA YA TRELA ILIYOKUWA IKISAFIRISHA KUPATA AJALI

Baadhi ya wananchi waliokuwa karibu na Hoteli ya Ole Sereni kwenye Barabara ya Mombasa siku ya Ijumaa, Septemba 23, waliangukia zare ya kupata unga wa bure wakati huu uchumi unavyowalemea wengi. Trela hiyo iliyokuwa imebeba unga wa mahindi ilipata ajali na kuvutia wapita njia. 

 Bela za unga zilianguka kutoka kwenye trela hiyo na kutapakaa barabarani, na kuvutia wakaazi wa eneo hilo waliowacha shughuli zao na kuanza kupora unga huo wa mahindi. 

Wenye magari walinaswa kwenye video za wanagenzi wakipakia bele hizo kwenye magari yao, huku wengine wakiwakodi wana bodaboda waliyosubiri kusafirisha mali. 

 Inaaminika kwamba trela hiyo ilikuwa imepita uzani unaohitajika kusafirisha mzigo huo, na kuifanya kuwa vigumu kwa dereva huyo kuithibiti kati ya 'interchange' ya Mombasa Road na Southern Bypass. 

Haijabainika ni kampuni ipi iliyokuwa ikisafirisha unga huo. 

Tukio hili linajiri wakati ambapo taifa linashuhudia mfumko wa bei ya unga wa mahindi, unaozwa kwa kati ya shilingi 200 na 250 kwa pakiti ya mbili. 

Maisha yamekuwa magumu kwa wengi wanaotegemea bidhaa hiyo, tangu serikali iondoe ruzuku ya unga hivi majuzi. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.