ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 23, 2022

NYUKI WAMVAMIA MLEVI NA KUMUUA SHAMBANI.

 


Mwanamume mwenye umri wa kati kutoka eneo la Gaturi kaunti ya Murang'a ameaga dunia baada ya kuvamiwa na kundi la nyuki. 

 James Wambu anasemekana alikuwa anatembea akitokea sokoni alikokuwa amekwenda kubugia pombe Jumanne, Septemba 20 jioni, wakati alilemewa kutokana na kulewa chakari na kulala katika moja ya shamba jirani.

 Kwa mujibu wa mashahidi, kulikuwa na vijana ambao walikuwa wamekwenda kuvuna asali katika shamba hilo ambako mwendazake alikuwa amelala. 

Katika harakati hiyo, vijana hao walilemewa na nyuki na kukimbia ili kuokoa maisha yao lakini Wambu ambaye alikuwa amelewa chakari, alishindwa kujinusuru.

 "Mahali ambapo wanaume hao walikuwa wakilina asali ni mita chache kutoka ambapo mwathiriwa alikuwa amelala."

 “Wahalifu hao walikimbia na kumwacha Wambu akiwa amelala chini na nyuki wakamvamia na kumwacha mahututi” alisema mmoja wa walioshuhudia. 

Chifu msaidizi wa eneo hilo Peter Gethi alipokea simu kutoka kwa wakazi wakimtaarifu kuhusu kisa hicho na wakati alipofika katika eneo la tukio, Wambu alikuwa tayari ameangamia.

 "Tulifahamisha polisi waliokuja kuchukua mwili huo na kuupeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti walipokuwa wakianza uchunguzi wa tukio hilo," Gethi alisema. 

Familia ya marehemu sasa wanashinikiza haki itendeke kwa jamaa wao wakidai kuwa wanaume waliokwenda kuvuna asali wangeliwazia kumuondoa mahali hapo kabla ya kuendelea na misheni yao. 

KUTOKA Kakamega 

Mnamo Mei 2022, iliripotiwa kuwa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), katika taarifa yake ilifichua kuwa mganga alitumia nguvu zake za kichawi kuwasaka wezi wa mifugo na kuwafikisha polisi. 

Kwa mujibu wa DCI, mmiliki wa mifugo hiyo, Imbiakah, alimtembelea mganga huyo baada ya kukuta mifugo yake haipo. 

Polisi walisema baada ya mganga huyo kufanya uchawi wake, washukiwa waliotajwa kwa majina ya Hillary Momanyi, 22, John Bukhazio, 28 na Winston Mutiele, 20, waliibuka. 

Washukiwa hao walibeba mbuzi na ndama waliodaiwa kuiba huku kundi la nyuki wakiwavamia mikono.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.