ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, September 22, 2022

WAKULIMA ZAIDI YA 1200 WACHANGAMKIA FURSA YA KILIMO CHA VANILLA ZANZIBAR.

 Na Victor Masangu,Zanzibar

Zaidi ya wakulima 1200 wamejitokeza kuwekeza katika kilimo cha zao la vanilla visiwani Zanzibar kwa lengo la kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini.

Wakulima hao wameamua kuungana na kujikita zaidi katika kilimo hicho ambacho wanaamini kitaweza kuleta mabadiliko chanya ya kuchochea ongezeko katika pato la Taifa pamoja na kuleta maendeleo kwa mkulima mmoja mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Vanilla International Limited Saimon Mkondya ambao walifanya ziara kwa ajili ya kutembelea na kunionea mashamba hayo ya Vanilla alisema lengo kubwa ni kuwasaidia wakulima kujikwamua kiuchumi.

"Kilimo cha zao hili la Vanilla kinasaidia Sana wakulima na kwamba kitaweza kuleta mabadiliko chanya zaidi ya kimaendeleo pamoja na kuchangia katika pato la Taifa kwa hiyo ni zao muhimu sana na linatajwa kuwa zao namba mbili kwa Bei kubwa duniani,"alisema Mkurugenzi huyo.

Aidha mkurugenzi huyo alibainisha kuwa kwa Sasa wamefanikiwa kuwapa ajira vijana wapatao 270 na kuwahimiza vijana wengine kushiriki kwa wingi katika kilimo cha zao Hilo.

Kwa upande wake kijana mmoja anaefahamika kwa Jina la Mohammed Mzee miaka 27 Mkazi wa Zanzibar  ameeleza kuwa ameacha kutumia Dawa za Kulevya aina ya Bangi mara baada ya kushiriki katika Kilimo cha Vanila ambacho kimebadilisha Maisha yake.

Ameeleza kwa takribani miaka 10 amekuwa akitumia bangi pamoja na kuishi maisha ya maskani ambapo hakuwa na muelekeo katika Maisha yake.
 
“Kiukweli sikuwa kwa Miaka mingi nilikuwa naishi maisha ya Maskani na kutumia Bangi ila baada ya kushawishiwa kujiunga na Kilimo cha Vanila nimeacha kutumia na sasa naelewa mustakabali wa Maisha yangu,” ameeleza.


Ameongeza kwamba kilimo hicho kina mfanya anakuwa anakuwa na Shughuli nyingi na kukosa muda wa kukaa Maskani na kutumia bangi na starehe nyingine.

Ameeleza kwa sasa anauhakika wa kuingiza kiasi kisichopungua Laki 350 na kuendelea baada ya kuingia katika kilimo hicho ambapo anashirikia katika shamba la Vanila Internation Limited Zanzibar huko bungi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.