ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 21, 2022

RAILA NA MARAFIKIZE WALIVYOSAKATA NGOMA USIKU KUCHA WAKISEMA NI YA MWISHO KAMA RAIA.

Tweet

Conversation

Video ya Raila Odinga, na Suleiman Shabhal miongoni mwa viongozi wengine wa kisiasa imezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii.  

 Baadhi ya wale ambao wako na Raila ni katibu wa muungano wa wafanyakazi nchini COTU Francis Atwoli, Peter Kenneth, mbunge wa Jubilee Maina Kamanda na Suleiman Shahbal. 

Kundi hilo liko katika sehemu ambapo inaaminika wanafuatilia matokeo ya uchaguzi wa urais ambayo yanaendelea kutangazwa na vyombo vya habari baada ya kujumuishwa. 

Kwenye video hiyo, Raila anaonekana akiwa amevalia suti licha ya kuwa ni usiku na hivyo kutoa ishara ya mtu aliye tayari kwa shughuli rasmi. 

Aidha mkononi anaonekana na simu ambapo ni kama alikuwa amezungumza na mtu fulani kabla ya kusisimka na kaunza densi. 

Baadhi ya marafiki alio na wao wanasema kuwa watu wanengue mwili vizuri hapo kwa sababu ndiyo ya mwisho akiwa bado raia. "Densi ya mwisho akiwa raia," mmoja alisema kuashiria kuwa alikuwa na imani kwamba kiongozi huyo wa ODM ataibuka mshindi wa urais. 

Video hiyo ilipakiwa mtandaoni na mwanahabari Jamal Gaddafi na nukuu za baadhi ya komenti zinasema: "Nafurahi nikiona Baba ana Furaha pia. Nani anacheka mwisho?" 

Tazama video hapa chini: Kauli za Wakenya 

@nandiThembi aliandika: "Huoni wanafanya sherehe ya mwisho kama Raia! Kesho hatakuwa Raia!" 

@Abdulmoduor aliandika: "Mimi nafurahi pia Baba anapofurahi." 

@elmer__254 aliandika: "Acha Jamaa akalie hio Kiti amesumbukana ya kutosha." 

@IreneKahiga1 aliandika "Furaha sana"

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.