Watoto wanne wamefariki dunia baada ya nyumba kuungua moto wakiwa ndani katika Kijiji cha Ngage Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara.
Akizungumza leo Jumatano Mei 4, 2022, Diwani wa Kata ya Loiborsoit, Siria Kiduya amesema tukio hilo limetokea jana mchana.
Kiduya amesema ajali hiyo pia imejeruhi mtu mmoja ambaye ni bibi wa watoto hao waliofariki.
Amesema kuwa watoto watatu walifariki papo hapo huku mmoja akifariki baada ya kupelekwa hospitalini.
"Watoto watatu walifariki dunia papo hapo na bibi akajeruhiwa na mtoto mwingine walipelekwa hospitali ya KCMC ya Moshi Mkoani Kilimanjaro," amesema Kiduya.
Amesema chanzo cha ajali hiyo ni bibi huyo, Anna Kipututu kutumia petroli ili kuwaua kunguni waliokuwa kwenye kitanda chao.
Amesema baada ya bibi wa watoto hao kumwagia petroli katika kitanda aliwasha moto ili kuwaua kunguni na moto ukaunguza nyumba wakiwa ndani.
Mkuu wa wilaya ya Simanijiro, Dk Suleiman Serera amethibitisha vifo hivyo na kutoa pole kwa wananchi wa kijiji hicho.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.