Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akizungumza wa Baraza hilo la Eidy Wilayani Kibaha.
Sheikh mkuu wa Mkoa wa Pwani Hamisi Mtupa akitoa maelezo wakati wa baraza hilo la Eidy lilifanyika Wilayani Kibaha.
Sheikh mkuu wa Mkoa wa Pwani Hamisi Mtupa akitoa maelezo wakati wa baraza hilo la Eidy lilifanyika Wilayani Kibaha.
Baadhi ya wazee maarufu wa dini ya kiislamu pamoja na waamini wengine wakiwa katika Baraza hilo wakifuatilia.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka ameungana kwa pamoja na waamini wa dini ya kiislamu katika Baraza la sikukuu ya Eid ambapo ameahidi kuchangia mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Bakwata Wilaya ya Kibaha.
Koka ametoa kauli hiyo wakati wa sherehe za Baraza hilo ambalo limefanyika katika shule ya msingi iliyopo kata ya Visiga Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani ambapo limehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa dini na serikali.
Alisema kwamba ofisi yake imekuwa bega kwa bega katika kushirikiana na Bakwata Wilaya tangu mwaka 2017 katika kuandaa Mabaraza hayo ya Eid lengo ikiwa ni kuweza kukutana kwa pamoja baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
"Mimi ofisi yangu imekuwa mstari wa mbele katika kuboresha mahusiano mazuri na wenzetu wa Bakwata bila kujali itikadi zozote za kidini kwa hivyo nimeamua kuchangia mifuko 100 ya saruji ambayo nina Imani itaweza kuleta mwanzo mzuri katika kuanza ujenzi,"alisema Koka
Aidha ameongeza kuwa pamoja na Mambo mengine ataendelea kushirikiana na viongozi mbali mbali wa dini katika kuchochea zaidi kasi ya maendeleo kwa wananchi wa Jimbo lake la Kibaha mji ikiwemo miundombinu ya barabara maji,umeme,afya pamoja na Mambo mengine.
"Nampongeza Sana Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo tangu aingie madaraka ameweza kutoa fedha nyingine ambazo zimesaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa,zahanati,vituo vya afya pamoja na Mambo mengine mbali mbali,"alisema
Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Pwani Hamis Mtupa aliwataka waamini wa kiislamu kutumia fursa mbali mbali walizonazo katika kuwasaidia watu wenye mahitaji wakiwemo wajane pamoja na watoto yatima.
Sheikh Mtupa aliongeza kuwa waislamu wanatakiwa kuwa wakarimu katika kipindi chote na sio mpaka uje mfungo wa mwenzi mtukufu wa Ramadhani na wanapaswa kuwa upendo ili kupata baraka kwa mwenyezi Mungu.
Pia alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini kwa upendo na moyo wake wa kujitolea katika kushirikiana katika Mambo mbali mbali ya kimaendeleo pamoja na kuungana na waislamu katika mambo mbali mbali.
Katika hatua nyingine aliziomba kamati za ulinzi na usalama kuendelea kuweka ulinzi madhubuti ili kudumisha hali ya ulinzi na usalama na kuepuka vita na machafuko Kama nchi nyingine.
Naye Sheikh wa Wilaya ya Kibaha Said Mtunda alitumia fursa hiyo kimshukuru Mbunge kwa mchango wake na kuwataka waislamu kuepuka kabisa na vitendo vya kufanya fujo na badala yake wajikite zaidi katika kutenda Mambo mema.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.