ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 26, 2018

WAZIRI MWAKYEMBE: SIDO WASAIDIENI WAJASILIAMALI WA TABORA KUPATA TEKNOLOJIA YA KISASA YA KUKAUSHIA BIDHAA.


 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (wakwanza kulia)  akitizama mboga za majani zilizokaushwa na kuhifadhiwa  katika paketi kwa ajili ya kuuzwa alipotembelea leo banda la wajasiriamali kutoka kikundi cha Amka Group cha Tabora Mjini kushoto ni Mjasiriamali wa kikundi hicho Bi.Anna Shango ambao wameshiriki maonesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji  linaloendelea Mkoani Tabora (wapili kulia) ni Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe.Joseph Kakunda uwanja wa Jeshi.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe  akitizama uyoga uliyokaushwa na kuhifadhiwa  katika paketi kwa ajili ya kuuzwa alipotembelea leo banda la wajasiriamali kutoka Mwamko Women Group kutoka Halmashauri ya Sikonge anayetoa maelezo ni Bi.Joyce Robert ambao wameshiriki maonesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji  linaloendelea Mkoani Tabora uwanja wa Jeshi.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati)  akitizama viungo vya mbalimbali vya chakula vilivyosagwa na kuhifadhiwa  katika vikopo kwa ajili ya kuuzwa alipotembelea leo banda la wajasiriamali kutoka Wilaya ya Uyui ambao wameshiriki maonesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji  linaloendelea Mkoani Tabora katika uwanja wa Jeshi.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (wakwanza kulia)  akitizama sabuni ya kuogea iliyotengenezwa na mjasiriamali  Bi.Neema Paulo na amempongeza  kwa kuweka picha yake  kuthibitisha ubora wa sabuni hiyo  alipotembelea banda la wajasiriamaliwa wa Wilaya ya Kaliua  leo kilichoshiriki maonesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji  yanayofanyika Mkoani Tabora katika uwanja wa Jeshi.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (wakwanza kushoto)  na Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe.Joseph Kakunda (katikati) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Aggrey Mwanri wakifurahia maziwa yanayotengenezwa na Neema Brand mjasiriamali mdogo wa Mkoa huo leo walipotembelea Maonesho ya wajasiriamali waliyoshiriki maonesho  ya Jukwaa la Fursa za Biashara  katika uwanja wa Jeshi linaloendelea Mkoani hapo,kushoto ni Bi.Sameera Sumar mmilikiwa biashara hiyo.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kushoto)  akitizama kiatu cha kiume kilichotengenezwa kwa ngozi  kwa ustadi mzuri  na mmoja wa wajasiriamali  wa mkoa wa Tabora  Bw.Baraka Vuzuka leo alipomtembelea maonesho ya wajasiriamali  yanayoendelea  katika Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji katika uwanja wa Jeshi .
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kushoto)  akitizama  zulia lillofumwa kwa mikono na Mjasiriamali  Bw.Hassan Rashid (kulia) kwa kutumia mikono  na mifuko ya sandarusi iliyokwisha kutumika na nzuri  leo  alipotembelea maonesho ya wajasiriamali  waliyoshiriki Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji  linaloendelea Mkoani Tabora katika uwanja wa Jeshi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.