Mgodi wa Buzwagi maisha yake ni mafupi na siyo siri kwamba ndani ya miaka miwili ijayo mgodi huo hautokuwa ukizalisha dhahabu tena.... Kupitia hilo Serikali imeitaka kampuni ya Acacia kuandaa na kuwasilisha haraka mpango mpya wa urejeshaji mazingira katika hali yake ya kawaida baada ya kusitisha shughuli za uchimbaji dhahabu katika mgodi wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama ifikapo mwaka 2020.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipofanya ziara katika mgodi huo kukagua shughuli zinazoendelea mgodi hapo na kugundua kuwa fedha iliyotengwa kwaajili ya kurudishia mazingira katika hali yake haiendi sanjari na uharibifu wa mazingira uliofanywa wakati wa uchimbaji madini (Ni fedha ndogo).
Imetajwa kuwa ili kujaa maji kwa moja ya shimo kubwa lililoachwa wazi itachukuwa miaka zaidi ya 100.
Naibu Waziri Doto Biteko (katikati), akifafanua jambo wakati akikagua shughuli mbalimbali katika mgodi wa Buzwagi.
Naibu Waziri Doto Biteko akielekea kukagua sehemu ambapo mchanga wenye madini (makinikia) umehifadhiwa ndani ya mgodi wa Buzwagi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.