ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 26, 2018

SAUTI - JAFO ATILIA SHAKA KIWANGO CHA FEDHA UJENZI MRADI WA KITUO KIKUU CHA MABASI NJOMBE



NJOMBE.

Waziri wa nchi ofisi ya rais serikali za mitaa na tawala za mikoa TAMISEMI Sulemani Jafo  ameonyesha kutoridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa awamu ya tatu wa kituo kikuu cha mabasi cha mkoa wa Njombe ambacho licha ya kuanza kujengwa 2013 hakijakamilika hadi sasa na kutoa agizo kwa mkandarasi kuhakikisha anakamilisha ujenzi huo ifikapo januari 7 , 2019.

Pamoja na kutoa agizo hilo waziri Jafo wakati akikagua ujenzi wa kituo hicho unaogharimu zaidi ya Bil 10 hadi kukamilika kwake chini ya ufadhiri wa benki ya dunia amemuagiza mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka kufanya uchunguzi wa kina juu ya thamani ya fedha inayotumika katika awamu ya tatu ya ujenzi huo ambayo itahusisha ujenzi wa Kituo cha daradara, Vibanda vya biashara na  Jengo la Utawala unaogharimu zaidi ya bil 5.7.

Amesema anashangazwa kuona kiasi kikubwa cha fedha kinatumika ujenzi huo na kumtupia lawama Eng Mshauri wa mradi huo unajengwa na kampuni ya HAINAN INTERNATIONAL Didas Joseph kwa madai ya kukosa uzalendo wa usimamizi wa miradi ya serikali licha ya kuajiliwa na serikali.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka anasema licha ya kufikia hatua nzuri katika utekelezaji wa awamu ya kwanza na pili lakini bado kumekuwa ujenzi wa chini ya kiwango kwa kuwa kumekuwa na nyufa nyingi katika mejengo na eneo la parking hali ambayo inaonyesha mradi huo uko chini ya kiwango na kuahidi kujipa muda wa uchunguzi zaidi kubaini madudu yaliotendeka.

Akifafanua sababu iliyopelekea kutokea kwa nyufa hizo na hatua zilizochuykuliwa Eng mshauri wa Mradi huo Didas Joseph amesema ni kutokana na msingi kutowekewa expernsion joint.

Pamoja na yote waziri Jafo ameagiza ifikapo January 7 Mwakani kituo hicho kiwe 
kimekamilika na kukabidhiwa.

TAARIFA YA AMIRI KILAGALILA KUTOKA NJOMBE

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.