GSENGOtV
Watu nane wameripotiwa kufa kwa kuteketea kwa moto na wengine wanne kujeruhiwa katika ajali ya gari mbili aina ya Hiace zilizogongana uso kwa uso na kusababisha gari hizo kuungua kwa moto na kuteketea. Ajali hiyo imetokea majira ya 9:30 Alasiri kwenye Kijiji cha Komaswa wilayani Tarime Mkoa wa Mara.
Kamanda Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya Henry Mwaibambe amesema kuwa hadi sasa idadi kamili ya watu waliokufa katika ajali haijajulikana ila taarifa za awali zinasema watu wanane wamefariki kutokana na ajali hiyo huku Chanzo cha ajali bado hakijajulikana
Ofisi ya Mbunge Jimbo la Tarime Mjini inapenda kutoa salamu za pole kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki waliopoteza watu wao katika ajali ya Gari ndogo mbili zilizogongana maeneo ya Komaswa na kuungua Moto na kusababisha Vifo kwa watu 10 waliokuwa wakutumia usafiri huo.
Ofisi ya Mbunge Tarime Mjini inawaombea Majeruhi wote Mkono wa uponyaji wa Mwenyezi Mungu ukapate kuwa juu yao na kupona haraka.
Baba wa Mbinguni atutie nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Imetolewa na:-
Peter Magwi Michael
Katibu wa Mbunge
Jimbo la Tarime Mjini.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.