ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 28, 2018

NAIBU WAZIRI MANYANYA AKUTANA NA BALOZI WA NIGERIA NCHINI.


 Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya kwenye kikao na balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. SahabuIsah alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar-es-salaam. Mhandisi Manyanya na mgeni wake wamezungumza mambo mbalimbali yanayohusu uwekezaji baina ya nchi hizo mbili. Kushoto (sutiyablu) niKatibuMkuu wa Wizara hiyo Profesa Joseph Bchweishaija.


Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Stella Manyanya, kwenye picha ya pamoja na balozi wa Nigeria nchini Tanzania, Mhe. SahabuIsah baada ya kumaliza mazungumzo yaliohusu uwekezaji wa nchi ya Nigeria nchini. Kushoto kwa Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Joseph  Bchweishaija. 


Naibu Waziri Manyanya Akutana Na Balozi Wa Nigeria Nchini.
Naibu Waziri Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya  leo amefanya mazungumzo na balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. Sahabu Isah kuhusu mambo mbalimbali ya uwekezaji nchini.

Katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ofisi ndogo za wizara hiyo Jijini Dar-es-salaam, Naibu Waziri Manyanaya na mgeni wake wamezungumza masuala mbalimbali ya uwekezaji ikiwemo uwekezaji wa uliofanywa na kampuni ya kuzalisha saruji ya Dangote.

“Tumefurahi kumuona balozi amekuja kututembelea na kufuatilia masuala ya uwekezaji  yanayohusu nchi yake”. Amesisitiza Mhe. Manyanya.

Mhe. Manyanya ameeleza kuwa kupitia kikao hicho wameweza kubalishana uzoefu katika masuala ya maendeleo ya nchi zote mbili.

Mhe. Waziri amemuhakikishia balozi huyo wa Nigeria kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi ya Nigeria katika masuala ya Uwekezaji na pia wizara yake iko tayari muda wowote kumokea endapo atakutana na changamoto yeyote.

Mbali ya kumhakikishia uhsirikiano, mheshimiwa Manyanya pia alitoa shukran za serikali kwa uwekezaji uliofanywa na nchi ya Nigeria “sisi tunafurahi kumuona Dangote amewekeza, na tungependa uwekezaji wake uendelee ili watanzania waendelee kufaidika na uwekezaji huo”, aliongeza mhandisi Manyanya.

Kwa upande wake Mhe. Sahabu amehaidi  kuendeleza ushirikiano uliopo baina na nchi hizo mbili na amefurahishwa na hatua za serikali za kutatua changamoto za wafanyabiashara mbalimbali kutoka Nigeria waliowekeza nchini.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.