Watu wanne wamefariki dunia na 11 kujeruhiwa baada ya kupata ajali mbaya ya gari la abiria walilokuwa wakisafiria kutoka Arusha kuelekea Mbeya mara baada ya dereva kushindwa kulimudu wakati akikata kona kwenye eneo la Mlima Haraa wenye kona kali kata ya Bonga mjini Babati.
Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Agustino Senga amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 3:15 asubuhi ya leo Oktoba 8-2018 katika Bara bara ya Babati-Dodoma ambapo gari la Abiria kampuni ya Arusha Express lenye namba za Usajili T 750- BYQ Scania likitokea Arusha kuelekea mkoani Mbeya lilimshinda dereva huyo aliefahamika kwa jina Kennedy Shayo kurudi upande wa pili wa kulia baada ya kukata kona ya haraka katika eneo lenye mlima na kona nyingi kisha kupinduka na kusababisha vifo na majeruhi kumi.
Waliofariki ni kondakta wa gari hilo Nassibu Ramadhani (43) mkazi wa Morogoro, Salvatory Thomas mkazi wa Haraa Babati,Laurent Mwanyabala mkazi wa Mbeya (46)Janefredy Mushi,ni mwanafunzi (21) mkazi wa Galapo Babati.
Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, Agustino Senga amefika katika eneo la tukio na kuthibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba dereva wa gari hilo lililokuwa limebeba abiria 56 alikimbia kusikojulikana baada ya ajali.
“Tutamtafuta dereva popote alipo kamahatojisalimisha itihada za kumtafuta dereva zinafanyika na chanzo cha ajali ni kushindwa kulimudu gari kwenye kona.” alisema Kamanda Senga.
Miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Babati Mrara kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.