Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akieleza maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi wakati akizungumza na wadau wa zao la kahawa kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Isingiro Wilayani Kyerwa, Leo 10 Julai 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Wadau wa zao la kahawa wakifatilia kwa makini mkutano uliowakutanisha wadau wa zao hilo uliofanyika katika ukumbi wa Isingiro Wilayani Kyerwa, Leo 10 Julai 2018.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa zao la kahawa kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Isingiro Wilayani Kyerwa, Leo 10 Julai 2018. Wengine pichani kulia ni waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Mhe Salum Kijuu.
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na wadau wa zao la kahawa kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Isingiro Wilayani Kyerwa, Leo 10 Julai 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Tizeba wakikagua na kuzungumza na viongozi wa Chama Cha Msingi cha Karukwanzi Wilayani Kyerwa, Leo 10 Julai 2018.
Na Mathias Canal-WK, Kagera
Biashara ya kuuza Kahawa nje ya
nchi pasina kufuata utaratibu wa kisheria (magendo) imepigwa marufuku hivyo
atakayebainika kuendelea na biashara hiyo atachukuliwa hatua Kali za kisheria
ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Agizo hilo limehusisha pia zuio
la wananchi kuuza kahawa mbichi ingali bado shambani haijakomaa (Butula) kwani
kufanya hivyo ni kudhoofisha na kuzorotesha juhudi za muda mrefu alizotumia
mkulima wa kahawa na kumkosesha mapato stahiki.
Marufuku hiyo imetolewa na
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba Leo 10 Julai 2018 wakati akizungumza
na wadau wa zao la kahawa kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Isingiro
Wilayani Kyerwa.
Waziri Tizeba alisema kuwa ilani
ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 ambayo ndio mkataba wa
wananchi na serikali yao inatoa maelekezo ya kuwezesha upatikanaji wa Masoko ya
Mazao ya Kilimo kwa kuviimarisha na kuviwezesha vyama vya ushirika kuwa na
uwezo wa kutafuta masoko ya mazao ya wakulima ya ndani na nje kwa kuweka mfumo
madhubuti wa ukusanyaji, uchambuzi na uenezaji wa taarifa za Masoko na kutoa
elimu juu ya uongezaji thamani na biashara.
Alisema serikali itajitahidi
kutafuta bei nzuri ya zao la kahawa ndani na nje ya Afrika Mashariki ili
wananchi wapate faida na tija ya Kilimo huku akieleza kuwa wakulima wa kahawa
kote nchini hawawezi kuona mafanikio ya Kilimo hicho kwa kuendeleza biashara ya
magendo sambamba na biashara ya kahawa mbichi ikiwa shambani (Butura).
Alisema kumekuwa na malalamiko
mengi kwa wananchi hususani baadhi ya wakulima wa kahawa kuuza zao hilo nje ya
nchi kinyume na sheria kwa hoja ya kwamba wanauza bei kubwa kuliko ndani ya
nchi hivyo ili kutambua gharama zilivyo Kesho 11 Julai 2018 watakutana na
kufanya mazungumzo na Waziri wa Ushirika kutoka Uganda anayeshughulikia mambo
ya ushirika ili kujua kama kweli Uganda kuna wanunuzi wenye uwezo wa kutoa
kiasi kikubwa cha fedha kuliko wanunuzi wa Tanzania ili wapewe utaratibu bora
wa namna ya kuja Tanzania kununua kahawa.
Aidha, waziri Tizeba ameagiza
Wakulima waliouza kiasi kidogo cha kahawa wasilipwe kwa utaratibu wa benki ili
kuepusha usumbufu badala yake kwa wale wakulima waliolima hekari nyingi na
malipo yao yatahusisha kiasi kikubwa cha fedha walipwe kwa utaratibu wa njia ya
Benki.
Aliongeza kuwa mafanikio ya
Kilimo nchini hususani zao la kahawa ni lazima kuuza kupitia Vyama vya msingi
vya ushirika ambapo ilani ya Chama Cha Mapinduzi sura ya pili kipengele cha 21
(n) inaeleza jinsi sheria ilivyofanyiwa marekebisho na kuanzisha sheria mpya
ambayo imeanzisha tume huru ya ushirika ili kuwa na tija kwa wakulima kwa ajili
ya kuwapatia faida kubwa ya kuuza kupitia ushirika.
Sambamba na hayo pia Waziri wa
Kilimo Mhe Tizeba amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Ndg
Shadrack Mhagama kukamilisha haraka iwezekanavyo kiwanda cha kukoboa kahawa cha
Omkagando kilichozinduliwa na Mwenge wa Uhuru tangu mwaka 2016 kwa gharama za
serikali lakini mpaka sasa kimeshindwa kuendekezwa.
Katika ziara hiyo Waziri wa
Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe
Charles Mwijage wametembelea na kuzungumza na viongozi wa Chama Cha Msingi cha
Karukwanzi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.