ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 26, 2018

MAKONDA AMCHONGEA MKUU WA KITUO KWA KAMANDA MAMBOSASA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda jana amefanya ziara ya utatuzi wa kero na migogoro ya wakazi wa Buguruni ikiwemo ule wa Wananchi waliovunjiwa nyumba baada ya kujenga ndani ya eneo la reli.

RC Makonda amesema wananchi wanapaswa kuunga mkono juhudi za serikali za ujenzi wa Reli ya kisasa (standard gauge) ambayo inaenda kulifikisha taifa katika uchumi wa kati na kuitangaza Tanzania katika ramani ya Dunia hivyo amewasihi wananchi waliovunjiwa kuwa wavumilivu.

Aidha RC Makonda ameiomba kampuni hodhi ya rasilimali za reli RAHCO kuangalia uwezekano wa kuwapatia wananchi angalau njia za kupita ili kuwapunguzia mizunguko mirefu.

Katika ziara hiyo RC Makonda amemuagia Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa kumuhamishia kituo kingine mkuu wa kituo cha Polisi Buguruni kwa kuwa watu anaowaongoza hawamuamini.

Hata hivyo RC Makonda ametoa siku Saba kwa kigogo wa Bodi ya Mikopo kumkabidhi bajaji kijana alietambulika kwa jina la Jafari Raphael aliegongwa na gari na kigogo huyo na kupelekea ulemavu wa kukatwa mguu mmoja pasipo kulipwa fidia yoyote na kumfanya kijana huyo kugeuka kuwa mtu wa kuomba misaada huku kigogo huyo akiendelea kula maisha na familia yake.

Pamoja na hayo Makonda amepatia ufumbuzi kero ya muda mrefu iliyokuwa ikiwakabili Umoja wa Madereva wa daladala buguruni Chama waliokuwa wamezuiwa kuegesha magari eneo la Buguruni station ambapo  amewaagiza madereva hao kurudi katika eneo hilo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.