ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 10, 2018

KIONGOZI WA UPINZANI ATOROKA GEREZANI KWA KURUKA UKUTA WENYE ULINZI MKALI.


Vyombo mbalimbali vya habari Rwanda vimeripoti kuwa serikali imethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kutoroka kwa kiongozi huyo wa ngazi za juu ndani ya chama cha upinzani.

Hilary Sengabo amesema kuwa Twagirimana na baadhi ya wafungwa wengine wameweza kutoroka kwenye gereza hilo baada ya kufanikiwa kuruka ukuta lakini uchunguzi dhidi ya tukio hilo unaendelea.

Hata hivyo wanachama wa chama hicho cha FDU wameshindwa kukubaliana na maelezo hayo huku wakilihusisha tukio hilo na maswala ya kisia nakuonyesha kuhofia maisha ya Twagirimana kuwa hatarinini.

Kwenye maelezo yaliyotolewa hapo jana siku ya Jumatatu FDU imekuwa ikiuliza inawezekanaje Twagirimana kutoroka kwenye gereza lenye ulinzi wa hali ya juu.

Mnamo Septemba mwaka 2017, Twagirimana na wanachama wengine nane wa chama cha FDU walikamatwa kwa makosa ya kuunda genge la kihalifu wa kutumia silaha dhidi ya Serikali.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.