GSENGOTv
BASI LAACHA NJIA NA KUPARAMIA NYUMBA MWANZA
Basi dogo la abiria aina ya TATA lenye namba za usajili T 537 DLF mali ya kampuni ya Mkombozi limeropotiwa kuacha njia na kuparamia nyumba ya mmoja wa wakazi katika eneo la Nyakazunzu wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.
Chanzo cha tukio hilo kimetajwa kuwa ni mwendo kasi uliopita kiwango hali iliyomshinda dereva kuhimili na kujikuta akigonga nyumba hiyo.
Basi hilo lilikuwa likitokea Sengerema kuelekea Mwanza mjini.
Hata hivyo hakujaripotiwa madhara makubwa ikiwemo vifo.
Tutaendelea kukujuza undani wa taarifa hii kupitia ukurasa huu na vipindi tofauti tofauti vya @jembefm Mwanza
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.