GSENGOtV
LEO tarehe 10 Octoba, 2018 Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amepokea ugeni wa Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohra Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb (TUS) aliyetua mapema leo mchana majira ya saa saba na robo uwanja wa ndege wa Mwanza.
Akiwa na msafara wake wenye watu takribani 25, kiongozi huyo anatarajiwa kuwa mkoani hapa kwa muda wa siku 3, akiwa ameweka kambi yake ya mapumziko katika eneo la Wag Hill Lodge iliyoko Luchelele wilayani Nyamagana.
Aidha ziara ya kiongozi huyo imelenga kutoa baraka kwa waumini wa Jumuiya ya Bohra, kushiriki nao ibada sanjari na kujionea hali ya mazingira ya kiutalii na vivutio vilivyopo mkoani Mwanza.
Dkt. Syedna ametua mkoani hapa, akitokea India kupitia jiji la Nairobi nchini Kenya ambapo alikodi ndege ya moja kwa moja na kumfikisha jijini Mwanza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.