ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 10, 2018

WATU ZAIDI YA 50 WAFARIKI KATIKA AJALI YA BASI KENYA, MAGUFULI ATUMA RAMBIRAMBI.


Watu 50 wamefariki dunia nchini Kenya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupata ajali kwenye barabara kuu ya Nairobi-Kisumu.
Walioshuhudia wanasema kuwa ajali hiyo ilitokea leo mwendo wa saa kumi na moja alfajiri.
Ajali hiyo mbaya ilitokea katika eneo la Fort Ternan Kaunti ya Kericho.
Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ni miongoni mwa waliotuma salamu za rambirambi kwa Wakenya.
AMEANDIKA "Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali ya basi iliyotokea Kericho nchini Kenya na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 50. Nakupa pole Mhe. Rais Uhuru Kenyatta, familia za marehemu na Wakenya wote. Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema na majeruhi wapone haraka."
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi Kaunti ya Kericho, James Mogera, basi hilo lenye uwezo wa kubeba abiria 67, lilitoka barabarani baada ya dereva kushindwa kulimudu kisha kugonga vizuizi vilivyokuwa kando ya barabara na kubiringia mita 20 kwenye bonde.
Kwa mujibu wa Gazeti la Daily Nation, miongoni waliofariki ni watoto wanane wa chini ya umri wa miaka mitano.
Awali idadi ya waliofarini ilikuwa 40 lakini polisi walielezae hofu yao juu ya vifo kuongezeka kutokana na hali ya baadhi ya majeruhi kuwa mbaya.
"Bahati mbaya sana tumepoteza watu 51," Mkuu wa Polisi Kenya Joseph Boinnet ameiambia redio ya Capital FM.
Mmoja wa walioshuhudia anasema alisikia honi, ikifuatwa na mlio mkubwa wa breki, kisha akawasikia abiria wakipiga kelele.
Baadhi ya majeruhi wanatibiwa katika Zahanati ya Fort Ternan, huku wengine wakikimbizwa hadi kwenye Hospitali ya Kaunti mjini Muhoroni kwa matibabu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.