ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 9, 2018

JEH KAULI YA MHE. RAIS KUHUSU WAMACHINGA MWANZA IMEPUUZWA AU KUNA UKIUKWAJI WA SHERIA?



GSENGOtV

Maswali mengi yameibuka mara baada ya Wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama Wamachinga wa eneo la Sahara jijini hapa kuamriwa kutoweka katika eneo la Sahara jijini Mwanza.

Wafanyabashara hao wameshusha lawama kwa mamlaka husika wakidai kuwatelekeza,  baada ya gari lililokuwa likipita maeneo yao ya biashara kupaza sauti likiwaamrisha kukusanya vyote vilivyo vyao na kuondoka haraka eneo hilo.

Wakati gari la matangazo likipita siku ya jumapili polisi na mgambo nao walikuwa eneo hilo wakiwataka kuondoka haraka iwezekanavyo,  wakati huo huo wakiwakatia umeme ili kupisha ubomoaji wa mabanda yao ya biashara.

Athumani Husein Juma ambaye ni Katibu Mwenezi Machinga Mkoa wa Mwanza anasema adha waliyoipata imezaa hofu juu ya hatma ya maisha yao.

- Mwananchi yeyote aliyejaribu kuhoji alinyamazishwa.
- Biashara zimefungwa hatujui tunakwenda wapi na hatujui maeneo yatatengwa lini?
- Ndani ya viongozi wa wamachinga wanageukana, kuna wengine wamepewa fedha kulibariki hili.

Ester Mashamba anasema Nashangaa sana mtu kama mimi mama mwenye uchungu, kwanini hii biashara inafanyika kihuni, kwanini hawa viongozi wasituambie ukweli, kwanini tunahangaika hivi?

Nina mkopo, Nina marejesho, Nina watoto wanaohitaji kwenda shule, lakini kwanini tunauzwa kihuni?

ANAYE TAJWA KUWA MMILIKI WA ENEO ANASEMAJE?

Chungulia VIDEO.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.