Mtayarishaji wa Muziki nchini Pancho Latino amefariki dunia muda mfupi uliopita.
Producer Pancho Latino ambae alifanya kazi nyingi za mafanikio kwenye studio mbalimbali ikiwemo kwa Prince Dullysykes na Hermy B atakumbukwa kwa ufundi aliokuwa nao hata kupewa kazi ya kung'arisha kazi kali za wasanii wakubwa nchini kama Ay, Vannesa Mdee, Joh Makini, Nikki wa Pili, Baraka Da Prince na wengine kibao.
Pancho Latino maarufu kama (#Mafia), amefariki kwa ajali ya kuzama na maji Kisiwa cha Mbudya jijini Dar es Salaam, Taarifa zaidi zitafuata.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.