Mkuu
wa Wliaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo amekiri kuwepo kwa
migogoro mingi ya ardhi kwenye Wilaya hiyo, ambapo amesema migogoro hiyo
inaibuka kutokana na kutengenezwa na watu.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni akizungumza mbele ya Wachimbaji Kokoto katika eneo la Boko,ambalo linadaiwa kuvamiwa na wananchi huku wakiendeleza shughuli za uchimbaji bila kufuata utaratibu/sheria.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Daniel Chongolo akiwa na watalaamu wake wakiondoka kwenye eneo hilo la wachimbaji Kokoto eneo la Boko,mara baada ya kujionea hali halisi na kuamuru uchimbaji kokoto katika eneo hilo usitishwe mara moja,mpaka hapo watakapokutana siku ya Alhamisi na kuamua nini kifanyike.
Mmoja wa wachimbaji Kokoto katika eneo hilo akieleza jambo kwa mkuu wa Wilaya Mh.Daniel Chongolo (hayupo pichani),aliyefika kujionea halisi ya eneo hilo
DC Chongolo ametoa
kauli hiyo wakati alipotembelea eneo la Uchimbaji Kokoto katika eneo la
Boko jijini Dar es Salaam, eneo lililokumbwa na migogoro baina ya
Wawekezaji na Wachimbaji hao.
Akizunguma na Globu ya Jamii na
Michuzi TV, Mhe. Chongolo amesitisha shughuli za uchimbaji kokoto katika
eneo hilo mpaka watakapokaa kwa pamoja Novemba Mosi 2018, kati ya
Wachimbaji wa Kokoto,wamiliki wa eneo na Serikali ili kusuluhisha
mgogoro huo ikiwa sambamba na kuangalia namna ya kuendelea au kuacha
shughuli hizo.
Chongolo amesema katika maeneo hayo ya uchimbaji
watahakikisha yanakuwa na Leseni ya Manispaa, Leseni ya Madini, Cheti
cha TRA, Mazingira, Mikataba kwa Waajiriwa, Malipo ya ushuru wa Madini
kwa Manispaa na usajili katika uzalishaji Madini. "Kwenye haya maeneo ya
uchimbaji Kokoto wanachimba kiholela, uharibufu ni mkubwa sana, magari
yanapita juu chini wamechimba mashimo, mvua ikinyesha wanakimbilia
wanajificha kwenye haya mashimo, ikileta madhara kwa watu malalamiko
yote yanakuja kwa Serikali’’, amesema DC Chongolo.
Kwa upande
wake mmoja wa Wawekezaji katika eneo la Boko, Mwakilishi wa Kampuni ya
Usafirishaji na Uchimbaji wa Kokoto ya Al-Hushoom Evestment, Badi Lema
amedai wao ni wamiliki halali wa eneo hilo, amesema kuna Watu wamevamia
eneo hilo hivyo waliiomba Serikali ifike kwenye eneo hilo kujionea
uvamizi huo.
Badi amesema licha ya kulinda eneo hilo, Wavamizi
hao wameendelea kuingia kwenye eneo hilo kwa ajili ya kufanya shughuli
za uchimbaji wa kokoto. Hata hivyo moja ya Wananchi wanaofanya shughuli
hizo za Uchimbaji amedai kuwa eneo hilo wamepewa na Wazo, wamedai eneo
hilo walipewa kama Wananchi wa Boko. Pia baadhi ya Wachimbaji hao
wamedai kuwa ruhusa ya Uchimbaji Kokoto katika eneo hilo la Boko
wamepewa na Serikali ya Mtaa.
Baadhi ya Wachimbaji wa Kokoto wakiendelea na shughuli zao katika eneo
linalodaiwa kuvamiwa na watu hao,ikiwemo uvunjwaji wa sheria za utunzaji
mazingira,na utaraibu wa kuchimba kokoto hizoMkuu wa Wilaya ya Kinondoni akizungumza mbele ya Wachimbaji Kokoto katika eneo la Boko,ambalo linadaiwa kuvamiwa na wananchi huku wakiendeleza shughuli za uchimbaji bila kufuata utaratibu/sheria.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Daniel Chongolo akiwa na watalaamu wake wakiondoka kwenye eneo hilo la wachimbaji Kokoto eneo la Boko,mara baada ya kujionea hali halisi na kuamuru uchimbaji kokoto katika eneo hilo usitishwe mara moja,mpaka hapo watakapokutana siku ya Alhamisi na kuamua nini kifanyike.
Mmoja wa wachimbaji Kokoto katika eneo hilo akieleza jambo kwa mkuu wa Wilaya Mh.Daniel Chongolo (hayupo pichani),aliyefika kujionea halisi ya eneo hilo
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.