Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia elimu OR-TAMISEMI Ndugu Tixon Nzunda, akifungua mafunzo ya maafisa elimu kutoka Wilaya na Mkoa wa Singida juu ya mfumo wa upimaji utendaji kazi kwa njia ya wazi OPRAS jijini Dodoma katika ukumbi wa Land Mark (Picha na Atley Kuni- OR-TAMISEMI)
Mwakilishi kutoka Mradi wa Kuimarisha Mifumo ya Sekta za Umma PS3 anayeshughulikia Rasilimali watu Geoffrey Lufumbi, akitoa maelezo ya utangulizi juu ya madhumini ya mafunzo hayo.
Bibi Dorine Lutahanamala, akiuchangia mada kwakutaka ufafanuzi wa juu mfumo wa OPRAS katika mafunzo yalioanza leo jijini Dodoma.
Mmoja ya wawezeshaji wa mafunzo hayo ya OPRAS Bibi Anyangise Lupembe, akitoa mada wakati wa mafunzo hayo ya siku mbili jijini Dodoma.
Washiriki wa mafunzo wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wakati akifungua mafunzo hayo ambapo washiriki hao watalazimika kwenda kuwafundisha walio chini yao
Washiriki wa mafunzo wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wakati akifungua mafunzo hayo ambapo washiriki hao watalazimika kwenda kuwafundisha walio chini yao
“OPRAS Iwe nyenzo ya Mikaba ya
Utendaji kazi” Nzunda
Na.
Atley Kuni, OR-TAMISEMI.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia
elimu Tixon Nzunda, amesema imefika wakati Mfumo wa upimaji utendaji kazi
uliowazi (Open Performance Review Appraisal System-OPRAS) kutumika kama nyenzo
muhimu ya upimaji kazi wenye matokeo chanya.
Nzunda
amesema hayo hivi leo alipokuwa akifungua, mafunzo ya siku mbili kwa Maofisa
Elimu pamoja na Makatibu wa Tume ya Watumishi wa Walimu TSD jijini Dodoma
kutoka Halmashauri za Mkoa wa Singida.
“Mtumishi
wa umma anatakiwa kupimwa kwa kuangalia mambo mahususi muhimu katika utendaji
wake kama, umahiri wake, ubunifu wake na weledi wa kutumia taaluma yake katika
utekelezaji wa majukumu yake.”
Naibu
Katibu Mkuu Nzunda, alisema OPRAS isitumike kama fimbo ya kuwaadhibu watumishi
bali kuwasaidia kutatua changamoto ambazo zitabainishwa kulingana na kada
husika na mazingira ya utendaji kazi.
Ameongeza
kuwa katika mfumo wa zamani ambao ulikuwa wa siri, ulimnyima mtumishi kujua
kile kinacho jazwa na msimamizi wake wa kazi hali iliyochangia baadhi ya
wasimamizi kuwaadhibu watumishi kwa hila na chuki binafsi.
“Katika
mfumo wa sasa, Mwajiri/msimamizi wa kazi na mwajiriwa watakaa pamoja na
kukubaliana kulingana na vigezo vilivyokubalika kupitia fomu ya OPRAS na endapo
hawatakubaliana watakwenda kwa msuluhishi” alisema Nzunda na kuongeza, “inawezekana
mtumishi ameshindwa kufikia malengo kwa sababu amekwamishwa na kutokuwepo kwa
nyenzo lakini wewe msimamizi unataka kumuadhibu. hiyo sio sahihi”.
Naibu
Katibu Mkuu, amewataka Maafisa Elimu hao kukubali kubadilika na kuachana na
dhana za kizamani za kuishi katika mifumo ya kizamani na badala yake wapokee
mawazo chanya yatakayo saidia katika utendaji kazi.
Katika
hatua nyingine, Naibu Katibu Mkuu Nzunda ametumia fursa hiyo kuwaonya watumishi
walimu walio wezi wa mitihani na wale watakao bainika kufanya hivyo hatakuwa na
simile nao.
“Tunataka
kujenga heshma ya nchi, tunapojenga heshima ya nchi lazima suala la elimu lipewe
kipaumbele muhimu, hatuwezi kuwafundisha watoto wetu kuwa wezi kuanzia darasa
la saba halafu tunataka waingie katika soko la ushindani kimataifa hatutaweza”,
alisisitiza Nzunda
Nzunda
ameahidi kulisimamia suala la wizi wa mitihani kwa juhudi zake zote na katika
kipindi chake chote katika nafasi yake hiyo hatakuwa tayari kuona kadhia hiyo
inajitokeza nakusema yeyote atakaye thubutu hatavumiliwa, sheria za kazi
zitachukuliwa ikiwepo kufikishwa mahakamani.
“Wizi
wa mitihani ni kosa la kimaadili, tukikukamata, mbali ya kukupeleka tume ya
walimu kwa shauri la kiusuluhishi, hatutaishia hapo, tutahakikisha mbali ya kufukuzwa
kazi tutakupeleka mahakamani na hatimaye ufungwe jela” alisema Nzunda.
Awali
akitoa maelezo na malengo ya mafunzo, Mwakilishi kutoka Mradi wa Kuimarisha
Mifumo ya Sekta za Umma PS3 anayeshughulikia Rasilimali watu Geoffrey Lufumbi,
alisema katika utafiti uliofanyika kuhusu OPRAS Mwezi February 2017, ilibainika
asilimia 80 ya watumishi waliohojiwa walionesha kutofahamu jinsi ya kuweka
malengo sahihi ya utendaji kazi.
“Katika
tafiti tendaji tuliofanya kwenye mikoa miwili ya Dodoma na Iringa na Wilaya nne
tulibaini kuwa asilimia 40 walikuwa hawajazi kabisa OPRAS, asilimia 75 walisema
hawaoni faida ya OPRAS, aidha asilimia 100 ya Wakurugenzi waliohojiwa walisema
hawajazi fomu za upimaji kazi uliowazi za OPRAS”. Alisema Lufumbi.
Lufumbi
alisema ili mafunzo hayo yawe na tija ameomba Ofisi ya Rais TAMISEMI kupeleka
maelekezo maalum kwenye Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ya kwamba ifikapo tarehe 05 Jamuari, 2019 Wakuu wa Shule
za Sekondari na Msingi wawe wamewezeshwa kuwaelekeza walimu namna ya kujaza
OPRAS kwa kufuata mwongozo ulioboreshwa.
Serikali
ilianzisha matumizi ya mfumo wa upimaji kazi uliowazi na tathmini ya utendaji
kazi kupitia waraka namba 2 wa 2004 na kufuta mfumo wa zamani ambao ulikuwa wa
siri na wa vificho usiompa fursa mwajiriwa kutathiminiwa kwa uwazi na ambao
ulikuwa ukizorotesha uwajibikaji katika utumshi wa umma.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.