ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
“Alikuwa
hana tabia kama za Wajerumani za kutosalimiana yeye alikuwa anatabia ya
kusalimia kila mmoja na hata majirani huko nchini ujerumani wanatambua alama
aliyowaachia marehemu Gamba ni kusalimiana nao na hata baada ya kifo chake kila
mmoja alimkumbuka kwa tabia yake ya kuwasalimia na kuongea nao kwenye basi
akienda kazini na alipokuwa akirudi nyumbani kwake,”
Ni moja kati ya kauli zilizo chomoza hii leo wakati Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akiongoza mamia ya wakazi wa Kanda ya Ziwa waliojitokeza katika viwanja vya Ofisi za Chama cha Umoja wa Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) vilivyopo kata Isamilo wilayani Nyamagana jijini hapa, kuuaga mwili wa mwanahabari Issac Gamba aliyekuwa akifanya kazi Idhaa ya Kiswahili ya sauri ya Ujerumani (DW).
Mwanahabari huyo aliyekuwa mtangazaji wa michezo na burudani katika idhaa hiyo alipatikana akiwa amefariki dunia mjini Born nchini Ujerumani Alhamisi ya tarehe 18 Oktoba baada ya kutoonekana ofisini kwa siku mbili.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.