Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa
Mwanza Mhe.John Mongella ametekeleza agizo la Rais Mhe. Dkt. John Magufuli la
kuhakikisha anafuatilia kero za wafanyabiashara ndogo ndogo (machinga) na
kuzitafutia ufumbuzi.
Katika
kutekeleza agizo hilo, Mhe. Mongella amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya Sengerema Magesa Mafuru kuhakikisha anakutana na wafanyabiashara wadogo
(machinga) ambao walinyang’anywa matunda yao (nanasi) zao kwenye oparesheni ya
kuwaondoa barabarani ili walipwe fidia.
Hatua hiyo
ilijiri jana Agosti 18, 2018 baada ya Mhe. Rais Dkt. Magufuli akiwa njiani Mjini Sengerema akielekea
Chato mkoani Geita kwa ajili ya mapumziko, kutoa agizo kwa watendaji wa
halmashauri hiyo kutowasumbua machinga na badala yake wawache wafanye biashara
zao huku akiagiza watendaji nchini kujikita kutatua kero za wananchi.
Ni baada ya
Mhe. Rais Dkt. Magufuli kusimama kwa ajili ya kusalimiana na wananchi ambapo
wafanyabiashara ndogo ndogo walimueleza kero zao ikiwemo ukosefu wa maeneo ya
kufanyia biashara zao hatua inayosababisha kubugudhiwa na viongozi wa halmashauri.
Kufuatia
malalamiko hayo, Mhe. Rais Dkt. Magufuli alimuagiza Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.
John Mongella kufuatilia kero hizo na kuzitatua ambapo muda mfupi baadaye Mhe.
Mongella alikutana na viongozi mbalimbali wilayani Sengerema akiwemo Mkuu wa
Wilaya, Mkurugenzi pamoja na machinga kwa ajili ya kutekeleza agizo la Mhe. Rais
Dkt. Magufuli.
Meza za wafanyabiashara ndogo ndogo (Machinga) katika soko la Kisima cha Chumvi Mjini Sengerema ambalo limetengwa kwa ajili ya wafanyabishara hao. Hata hivyo baadhi ya wafanyabiashara wanagoma kuhamia katika soko hili kwa kile wanachodai ni kukosa wateja na hivyo kuendelea kufanyia biashara zao katika hifadhi ya barabara Mjini Sengerema.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.