ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, August 20, 2018

MBUNGE WA KWIMBA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA YA MAGUFULI.

MIMI SHANIF MANSOOR. MBUNGE WA JIMBO LA KWIMBA, PAMOJA NA FAMILIA YA NGU NA WATANZANIA WOTE NAPENDA KUTUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT JOHN POMBE MAGUFULI KWA KUFIWA NA DADA YAKE KIPENZI, MONICA JOSEPH MAGUFULI. 

Bi Monica amefikwa na mauti hospitali ya Rufan Bugando alipokuwa anapatiwa matibabu chumba cha uangalizi maalum (ICU)

Nimepokea kwa mshituko taarifa za msiba wa mama yetu Mpendwa MONICA.
Kwa niaba ya wana Kwimba tunaungana na familia ya Magufuli pamoja na wana Chato  wote kwenye maombi na dua zetu kuiombea familia utulivu na faraja wakati huu wa Majonzi.

Niko pamoja na Rais wetu mpendwa Mhe. JOHN POMBE MAGUFULI, katika kipindi hiki kigumu, MUNGU akutie nguvu na afya tele.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.