ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, August 20, 2018

MBARAWA ATOA MIEZI MI 3 KUKAMILISHA MIRADI YA MAJI WILAYANI KWIMBANA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV

WAZIRI wa maji na umwagiliaji  MAKAME MBARAWA, amezindua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyandiga wilayani kwimba mkoani Mwanza uliogarimu zaidi milioni 570 pamoja na kutembelea mradi mkubwa wa maji katika kata ya shirima uliokwamishwa na makandarasi wasio waaminifu wa zaidi ya bilioni 2.

Aidha MBARAWA, katika ziara yeke amemuahidi mbunge wa kwimba SHANIF MANSOOR, kukamilisha kwa haraka mradi huo utakaosaidi kuondokana na changamoto ya maji kwani unahudumia vijiji zaidi ya 14.

Akitengua kitendawili hicho cha maji kilicho dumu kwa zaidi ya miaka 5 baada ya mradi  huo mkubwa uliogarimu zaidi ya bilioni 2 kukwamishwa na wakandarasi wasio waaminifu.

 Akizungumza na wananchi wa kijiji cha shirima katika jimbo kwimba mkoani Mwanza MBARAWA, amewaahidi  wananchi waliokuwa wamekata tamaa yakupata maji safi kutoka ziwa victoria na kuahidi kupata maji ndani ya miezi 3 alisema MBARAWA,

Aidha Mhe. SHANIF MANSOOR,mbunge wa jimbo la kwimba amesema changamoto kubwa katika jimbo lake ni maji alisema MANSOOR, kutokana na mradi huo kuchelewa huwalazimu wananchi kutumia maji ya malambo ambayo sio salama kutumiwa na wananchi wake.
Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.