ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 11, 2018

WAZIRI KANGI LUGOLA ATEMBELEA KIWANDA CHA MAGEREZA UKONGA, JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimsikiliza Inspekta Carlos Hanga (kulia), wakati alipotembelea Kiwanda cha Magereza Ukonga, kinachojishughulisha na uchongaji wa thamani za ndani na ufumaji wa nguo, jijini Dar es Salaam. Waziri Lugola yuko kwenye ziara ya kikazi baada ya kuteuliwa kuongoza wizara hiyo. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akikagua ubora wa thamani inayotengenezwa katika Kiwanda cha Magereza, kilichopo Gereza la Ukonga, jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya kutembelea Jeshi la Magereza. Kulia ni Kamishna wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa. 

Inspekta wa Jeshi la Magereza, Carlos Hanga akitoa maelezo ya kiufundi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ambaye yuko katika ziara ya kikazi katika Kiwanda cha Gereza kilichopo Ukonga, jijini Dar esSalaam. 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akisalimiana na maofisa waJeshi la Magereza, baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi katika Chuo cha Magereza , kilichopo Ukonga, jijini Dar es Salaam. 
Waziriwa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akipita mbele ya Maofisa wa Jeshi la Magereza, baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi katika Chuo cha Magereza , kilichopo Ukonga, jijini Dar esSalaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.