NA ZEPHANIA MANDIA GSENGOtV
Baada ya serikali kuimarisha mapambano dhidi ya
biashara haramu ya dawa za kulevya,baadhi ya watu wanaamini zama ni zile zile
kwa tafsiri tu ilimradi mkono uende kinywani.ni tukio la aina yake, likiibua
mitazamo hasi kwa kila aliyelishuhudia ama kulisikia.
Gari la hospitali ya wilaya tarime iliyozoeleka
kubeba wagonjwa mahututi leo imenaswa wilayani bunda ikisafirisha shehena ya
dawa za kulevya aina ya mirungi kutoka wilayani tarime kwenda jijini mwanza
kutafuta soko.
Shehena hiyo imekamatwa wilayani bunda mkoani
mara ikiwa ndani ya gari hilo lililokuwa limewasha alama za kuonyesha kuwa na
mgonjwa.
Akizungumza baada ya kushuhudia shehena
hiyo,Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama,mkuu wa mkoa wa Mara ADAM MALIMA amewaonya wale wote
wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa mara JUMA
NDAKI jeshi hilo linawashikilia watu wawili akiwemo dereva wa gari hilo la
wagonjwa GEORGE MATAI ambaye licha ya kutakiwa kuchukua mgonjwa mahututi toka
hosptali ya Tarime na kumpeleka Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza
alitoa visingizio juu ya gari kutokuwepo na baadae kubainika akiwa na dawa za
kuleva wilayani Bunda huku akiwa amewasha alamu kuonyesha yupo na mgonjwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.