POLISI
KUFANYA OPERESHENI KALI VISIWA VYA ZIWA VIKTORIA.
Na. Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema Jeshi hilo litafanya Operesheni kali ya
kupambana na wahalifu katika maeneo ya Visiwa vilivyopo katika ziwa Viktoria
ili kuhakikisha kuwa wavuvi wanafanya kazi zao bila woga wala hofu ya kufanyiwa
uhalifu.
IGP Sirro ameyasema
hayo wakati akizungumza na Wananchi wa Kata za Kagongo, Nyasaungu na Kiriba
ambazo zipo katika Visiwa vilivyopo Ziwa Viktoria Mkoani Mara wakati wa ziara yake inayoendelea katika mikoa
ya Kanda ya Ziwa kwa lengo la kubaini changamoto za kiuhalifu na kuzipatia
ufumbuzi wa haraka ili wananchi waendelee kufanya kazi zao kwa Amani na
utulivu.
Amesema Jeshi hilo
limejipanga ipasavyo kuhakikisha kuwa kila mwananchi anafanya kazi zake salama
kwakuwa uwezo na nguvu wanayo na ndio maana uhalifu unaendelea kupungua hapa
nchini.
“Uhalifu wa kutumia
silaha ndugu zangu umepungua kwa kiasi kikubwa kwaiyo hata hao wanaotujaribu
huko ziwani nawapa salamu waache mara moja kabla ya moto mkali haujawafikia
mana hatuna mchezo tunapokutana na mhalifu hususani anayetumia silaha” Aisema
Sirro.
Kwa upande wake
Diwani wa kata ya Kiriba Msendo Nyamsora alimweleza IGP kuwa tatizo kubwa
linalowasumbua ni baadhi ya wahalifu ambao wanadaiwa kutoka nchi jirani za
Uganda na Kenya kuwavamia wavuvi wawapo ziwani huku vyombo vyao vya uvuvi
vikiwa vinapeperusha bendera za Tanzania ambapo aliziomba mamlaka husika
kusimamia kwa makini utaratibu wa kupeperusha bendera hizo.
Naye Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Juma Ndaki amesema
atahakikisha vikundi vya ulinzi shirikishi vinaimarishwa katika maeneo hayo ili
visaidiane na askari Polisi kufanya doria za mara kwa mara.
IGP anaendelea na
ziara yake katika mikao ya kanda ya ziwa huku akitumia usafiri wa Helkopta ili
kujionea kwa uhalisia maeneo hayo ili kuweza kuzipatia ufumbuzi changamoto za
uhalifu katika maeneo ya Visiwa vya Ziwa Viktoria.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.