ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, July 8, 2018

CUF YATANGAZA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI MDOGO WA MARUDIO


Chama Cha Wananchi CUF kimeweka bayana kwamba hakitoshiriki katika uchaguzi huu mdogo wa marudio uliopangwa kufanyika nchini kote Agosti 12 , 2018 baada ya Kamati ya Utendaji kufanya uchambuzi wake na tathmini.

Taarifa iliyotolewa leo na  Kurugenzi ya Habari –CUF Taifa na Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma ndg, Mbarala Maharagande imesema kwamba sababu za msingi za kutoshiriki uchaguzi huo ni pamoja na Mkanganyiko wa uongozi katika usimamizi wa uchaguzi huo uliojitokeza kutokana na mgogoro uliopandikizwa ndani ya CUF na Lipumba pamoja na washirika wake.

Maharagande  amesema kwamba CUF inaona ni busara kwa sasa kuelekeza nguvu na rasilimali zake chache zilizopo katika kushughulikia na kuupatia ufumbuzi mgogoro huu uliopandikizwa.

Pamoja na hayo chama hicho kimetoa wito kwa vyama rafiki vyote katika UKAWA kukaa pamoja kufikia muafaka na maridhiano na kusimamisha Wagombea bora, Imara, na madhubuti kugombea nafasi hizo zote.

Hata hivyo CUF inatoa wito kwa Viongozi na wanachama wake wote katika maeneo yote ya marejeo ya Uchaguzi kwa Tanzania Bara kushirikiana bega kwa bega na kuunganisha nguvu za pamoja na vyama rafiki vya UKAWA katika uchaguzi huu ili kuishinda CCM na vibaraka wake.

Katika kata 79 zilizotangazwa na Tume ya Uchaguzi Taifa, CUF imepoteza Kata 4 ilizokuwa inaziongoza kwa Madiwani wake kuhamia CCM - Kata mbili zipo manispaa ya Jiji la Tanga Mjini na Kata moja Mtwara Vijijini na Diwani mmoja Kufariki Wilaya ya Kwimba.

Siku ya jana Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), (upande wa Prof. Ibrahim Lipumba, Magdalena Sakaya alisema chama hicho kitashiriki uchaguzi wa ubunge katika majimbo ya Buyungu, Jangombe na kwenye Kata 79 zilizotangazwa na Tume.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.