ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 30, 2018

PICHA MAPOKEZI YA NDEGE YETU MWANZA.

 Hatimaye ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu kuanza safari zake tayari ndege hiyo imeanza kupasua anga na safari hii imetua jijini Mwanza. nchini Tanzania
 Viongozi wa dini, wakuu wa Serikali, wafanyabiashara, wakulima, wanafunzi na wadau aina nyingine wameonekana viwanjani hapa kuilaki ndege hiyo.
 Ndege hiyo ina uwezo kubeba abiria 262.
Ndege nyingine ambazo zilinunuliwa na serikali ya Tanzania ni ndege moja aina ya Bombardier Q400 Dash 8 NextGen , ndege 2 aina ya Bombardier CS300 zenye uwezo wa kuchukua kati ya abiria 137 na 150 .
 Salamu toka kwa mbunge wa Ilemela Angelina Mabula alikuwa ni mmoja wa abiria wa kwanza wa ndege hiyo.
 Rais Magufuli alikuwa ameahidi kwamba shirika hilo lingeimarishwa na ndege mpya kununuliwa mara baada ya kuingia madarakani.
 Wageni wameonekana kuwasili akiwemo aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Nyamagana Serikali ya Kikwete, Baraka Konisaga.
 Asalaam aleikum.
 Baba na mwana.
 Ulinzi na usalama eneo la tukio.
 'Gsengo tukioni' Ikiwa tayari ndege hii imeanza safari zake kwa mikoa ya Kilimanjaro na sasa Mwanza maeneo mengine ambayo ATCL inatarajia kuongeza safari zake ni Dodoma, Mbeya, Kigoma, Tabora, Mpanda, Kilimanjaro, Mtwara, Zanzibar, Pemba, Bukoba na Visiwa vya Comoro.
Kulingana na Boeing, 787 Dreamliner ni familia yenye teknolojia ya kisasa ,ndege zenye utendaji mzuri na vitu vipya vya kupendeza.
 Watu muhimu sana.

 Akizungumza na waandishi wa habari mapema tu baada ya kutua jijini Mwanza kuhusu viwanja ndege hiyo inavyoweza tua, Muongozaji wa ndege hiyo Kaptaini Richard Shaidi amesema ndege hiyo kwa sasa inaweza kutua Viwanja vya ndege vinne tu nchini Tanzania ambavyo ni KIA, Uwanja wa ndege wa Mwanza, Zanzibar na Uwanja wa Mwl. JK Nyerere jijini Dar es salaam.

Amefunguka pia kuhusu ubora wa ndege hiyo huku akieleza speed ya ndege hiyo na sifa zake za ndani ikiwa angani.
 Mbali na kuleta vigezo vya ndege kubwa katika ndege za wastani, 787 Dreamliner italipatia shirika la ndege la Air Tanzania ufanisi wa mafuta na mazingira ya utendaji, kwa kutumia chini ya asilimia 20 hadi 25 ya mafuta na asilimia 20 hadi 25 wa uchafuzi wa mazingira ikilinganishwa ndege nyengine zilizotumika awali.
 Kwangu yahitaji ujasiri wa kiwango cha juu.... Jeh kwako Unaweza......?
 MNEC wa wilaya ya Tarime ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu Kanda ya Ziwa C. Gachuma naye alitua na dege hilo.
 Salaam za wana Mwanza.
 Picha ya pamoja na viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali.
Picha na baadhi ya wanafunzi wawakilishi vyuo  mbalimbali mkoani Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.