Wafanyakazi wa Airtel kitengo cha huduma kwa wateja wakishangilia na Kombe lao mara baada ya kushinda nafasi ya kwanza kwenye bonanza la Airtel Familia lilifanyika mwishoni mwa wiki hii. Airtel imefanya bonanza hilo la lawafanyakazi ambapo wasichana toka vitengo mbalimbali ndani ya kampuni hiyo walishindani kupiga penati ambapo kitengo cha huduma kwa wateja waliibuka washindi kwa penati 6-5 dhidi ya kitengo cha Mipango na fedha cha Airtel.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso (watatu toka kushoto) akikabidhi zawadi ya kombe kwa washindi wa kwanza ambao ni kitengo cha huduma kwa wateja walipoibuka washindi kwa kukiladha kitengo cha fedha na mipango kwa golo za penati 6-5 wakati wa Bonanza la wafanyakazi wa Airtel lililofanyika mwishoni mwa wiki. Kitengo hicho pia watapata zawadi ya kwenye kupata chakula cha mchana kwenye hotel ya nyota tatu wote wakiwa wamelipiwa gharama zote na Airtel.
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Bw, Isack Nchunda akikabidhi zawadi ya kombe la mshindi wa pili kwa Nahodha wa timu ya kitengo cha Fedha na Mipango cha Airtel Bi Foibe Saimon mara baada ya kumalizika kwa bonanza la wafanyakazi wa Airtel lililofanyika mwishoni mwa wiki kwa lengo la kujenga afya na kuhamasisha wafanyakazi wa Airtel kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake.
Kushoto ni kocha wa timu ya kitengo cha fedha cha Airtel bw Sylivester Nsabi (Gadiola) na Nahodha wa timu hiyo Bi Foibe Saimon wakipokea kombe la ushindi wa pili toka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Bw, Isack Nchunda wapilitoka kushoto akiwa na Mkurugenzi wa kitengo cha Fedha Bw Nishant Mohan. Bonanza la wafanyakazi wa Airtel lililofanyika mwishoni mwa wiki kwa lengo la kujenga afya na kuhamasisha wafanyakazi wa Airtel kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake.
Mchezaji wa Kitengo cha Fedha cha Airtel Bi Foibe Simon akipiga penati dhidi ya kitengo cha huduma kwa wateja wakati wa Bonanza la Familia ya wafanyakazi wa Airtel lililofanyika kwa lengo la kujenga afya na kuhamasisha wafanyakazi wa Airtel kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake.
Meneja Rasilimali watu Pamela Mwandetele akijiandaa kupiga penati wakati wa bonanza Bonanza la wafanyakazi wa Airtel lililofanyika mwishoni mwa wiki kwa lengo la kujenga afya na kuhamasisha wafanyakazi wa Airtel kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake.
AIRTEL YA WASHIRIKI BONANZA KUJEGA AFYA
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma bora za Smartphone kupitia kitengo chake cha rasilimali watu wameandaa bonanza la michezo lililowashirikisha wafanyakazi wake wote kwa lengo la kujenga afya za wafanyakazi hao pamoja na kuongeza ushirikiano eneo la kazi.
Akiongea mara baada ya tamasha hilo kuisha Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu alisema “Airtel tunatambua jitihada za serikali zinazosisitiza kuboresha na kuweka mzingira rafiki sehemu za kazi, pia Airtel tunafahamu sana umuhimu wa michezo na mazoezi kwa afya za wafanyakazi wetu, Hivyo ndio maana tumeona ni vyema kukutana kwa michezo kama hivi ili kuwasaidia wafanyakazi kurelax na kubadilishana mawazo wakiwa katika mazingira tofauti”
Katika Bonaza hilo la muziki na mchezo wafanyakazi wengi walifurahia zaidi mchezo wa kupigiana penati ambao washiriki walikuwa ni wasichana wote kwa mgawanyo wa vitengo vyao vya kazi kikiwemo kitengo cha ofisi ya Mkurugenzi mkuu kinachoundwa na rasilimali watu na udhibiti huduma, kitengo cha masoko, huduma kwa wateja, kitengo cha mauzo, ununuzi na ugavi, pamoja na kitengo fedha na mipango.
katika mchezo huo ushiriki ulikuwa wenye uvutano mkubwa kwa mzunguko wa ngazi ya mtoano na kuwa wenye ushindani mkali zaidi pale ambapo walibaki vinara watatu ambao ni kitengo cha Huduma kwa wateja waliokichapa kitengo cha fedha na mipango kwa goli 6 huku wao wakiambuia goli tano na kuwafanya kitengo cha huduma kwa wateja kuibuka washindi wa ujumla na kubeba kombe la ushindi wa mchezo huo.
Kibacha alisema “Airtel kupitia ofisi ya Rasilimali watu bado wataendelea na programu nyingine nyingi za kuwajenga na kuwaweka watoa huduma na wateja kuwa karibu zaidi”
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Aitel Bw Sunil Colaso aliwapongeza washindi wa Bonanza hilo na kuwataka wafanyakazi wake kuzingatia sana umakini pale wanapohudumia wateja
“niliona mwanzo mlianza kushindania kawaida mno lakini baada ya ushindani kupamba moto wote mkawa makini na mkawa mnalenga kwelikweli mpira usieme nje, sasa mnapaswa umakini huo pia muuzingatie kwenye kutoa huduma kwa wateja wetu wote tunapaswa kuwa makini hivi hivi” alisisitiza Colaso
Mkurugenzi huyo pia alisema kwa kuwa Airtel inashirikiana na wadau wengi watahakikisha hawaishii hapo wanawakutanisha na watoa huduma ili wafurahie kuwa ndani ya familia ya Airtel
tutakutana na wadau watoa huduma mbalimbali wiki ijayo ikiwa lengo ni kuwasaidianaupatikanaji wa huduma mbalimbali ikiwemo afya ya kinywa na macho, kujua jinsi yakujipatia bidhaa bora za vifaa vya moto kama magari, jinsi ya kupata mikopo ya Nyumba, viwanja na hata jinsi ya kuweka insuarance kwenye baadhi ya mali zao” alisema Colaso
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.