ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 17, 2018

HIZI NDIZO NONDO ZITAKAZO MRUDISHA STANSLAUS MABULA BUNGENI 2020



GSENGOtV

Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula leo tarehe 16.07.2018 ameanza Ziara ya siku tatu kutembelea  vyombo mbalimbali vya habari, ziara itakayokoma mnamo siku ya jumatano (tarehe 18.07.2018)

Dhima ya ziara yake hiyo ni kujenga Mahusiano bora na taasisi hizo za upashaji habari na watendaji wake kwa ujumla. Mabula pia amepata fursa ya kushiriki baadhi ya vipindi na kuelezea utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM 2015-2020。

Mapema leo baada ya kufanya mahojiano na Kituo cha Radio Jembe Fm Mwanza, ikawa ni zamu ya Gsengo Tv, haya ni baadhi ya maswali yaliyohusika kwenye mahojiano:-

1. Ni miaka mitatu sasa umepewa dhamana na wananchi wa Nyamagana kuwa mtumishi wao, mtetezi wao, mtu ambaye unawasilisha changamoto zao kwa Serikali ili zifanyiwe kazi. Nini tofauti katika maendeleo ya Sekta ya miundombinu ya barabara kabla ya wewe kuingia madarakani na sasa.

2. Mnalaumiwa kuwa Nyakati nyingine miradi mbalimbali ya kimaendeleo kukwamishwa na nyie wanasiasa, kuwalea wananchi hata pale ambapo si sawa na nikinyume na sheria tulizojiwekea, mkihofia tu kupoteza KURA.

Wamachinga wanafanya biashara kwa uhuru katikati ya mji hata kupitiliza, na sasa wamevamia hifadhi ya barabara, halmashauri zinalipinga hili lakini ninyi wanasiasa mnaegemea upande wa wananchi mambo yanakwenda ndivyo sivyo, Jeh hili liko sawa kwa kwako?

3. Suala la ardhi na umilkishwaji limekuwa kimya muda mrefu, licha ya wananchi kupimiwa viwanja vyao lakini ni miaka miwili sasa kimya hawajapewa hati zao, mfano wananchi wa Kata ya Luchelele. kipi kiko nyuma ya hili?

4. Sekta ya michezo na uwanja wa Nyamagana lini majukwaa yatajengwa au ndiyo ntoleee?

MWISHO. 
Swali likawa juu ya historia ya Nyamagana na wabunge kutorejea baada ya miaka mitano, 5. Jeh Stanslaus Mabula nini kitakachomrudisha 2020 kuomba tena ridhaa ya wananchi?

MAJIBU YOTE NDANI YA KIDEO HAPO JUU.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.