RC Geita Mhandisi Robert Gabriel (mwenye kofia nyeusi) pamoja na wateja wakishuhudia uchomaji wa dhahabu yao.
Dhahabu baada ya kutoka kuchomwa ikisubiri kusafishwa kuondolewa uchafu
RC Geita akifurahia matunda ya uzalishaji dhahabu
Mikono ya RC Mhandisi Gabriel ikiwa imeshikilia vipande vya dhahabu
Mikono ya RC Mhandisi Gabriel ikiwa imeshikilia vipande vya dhahabu
RC Mhandisi Gabriel akitoka nje ya jengo la elution plant ya mwananyanzala
9.Picha ya mitambo (majiko) ya kuchomea carbon zenye dhahabu
Wafanya Biashara Njooni;
Elution Plant na Umeme Siyo Tatizo Mkoani Geita
Ni kauli ya Mkuu wa Mkoa wa
Geita, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel
alipofanya ziara ya kushtukiza na kujionea uzalishaji wa dhahabu katika Elution
Plant (viwanda vya kuchomea Carbon zenye Dhahabu) mjini Geita.
Mhe.
Mhanidisi Gabriel amefurahishwa na muitikio wa wamiliki wa
elution plant hizo kuongezeka siku hadi siku ambapo ametembelea eneo la Nyanza
lililoko Mbugani Mjini Geita lenye viwanda hivyo saba na kujifunza mengi
ikiwemo jinsi dhahabu hiyo inavyopatikana.
Mkuu wa Mkoa ameshuhudia
dhahabu yenye uzito wa Kilogramu moja na gramu mia mbili (Kg. 1.2) yenye
thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni Mia Moja (Tshs.100,000,000/=) ndani ya
dakika arobaini na tano (45) alizofika kwenye Elution Plant moja ya
Mwananyanzala, hali iliyompelekea kusema;
“ninadhani mmeona wenyewe, carbon za kilo mia nne mteja wa kwanza, mia
nne mteja wa pili tumepata kiasi hiki cha dhahabu, hii ni dalili njema kwa Mkoa
na hizi ni kutoka Elution moja tena kwa dakika hizo, sasa vipi kwa Elution
nyingine?. Ninataka fedha inayopatikana kwenye dhahabu irudi kwa jamii, ijenge
miundombinu lakini pia wafanya biashara wa Dhahabu njooni tuna Elution saba
hapa Nyanza eneo la Mbugani, hazina mzigo zinawasubiri mlete carbon lakini pia
Kamera za usalama zipo (CCTV Camera), hakuna haja ya kuogopa na Mkoa uko shwari
hakuna tatizo, Elution nyingine zinaendelea kujengwa s,gesi na transfoma za
kutosheleza mahitaji yenu tumekwishazipokea shaka ondoa sasa” alisisitiza.
Moja ya wateja kutoka Nyarugusu
Wilayani Geita (jina limehifadhiwa), alishukuru kwa namna ambavyo serikali
inavyohusika kuanzia hatua ya kwanza anaweka mzigo wake hadi hatua ya upimaji
kwani kwa kufanya hivyo hata yeye anaona hakuna nafasi ambayo ataibiwa mzigo
wake na kumpongeza Mkuu wa Mkoa na Serikali kwa ujumla kwa jitihada anazoendela
kuzifanya pamoja na wasaidizi wake kwa kuwa yeye kama mteja na Serikali ndiyo
huweka makufuli kwenye mitambo ya kuchomea dhahabu hivyo hana hofu ya kuibiwa
kama zamani.
Kwa upande wake moja ya
wamiliki wa kiwanda cha Jema Africa, Elution Plant iliyokuwa ikifanya shughuli
zake Mkoani Mwanza amesema, “kwakweli
ninaziona faida za kuja Geita, wateja ni wengi, tofauti na nilivyokuwa kule,
hivyobasi nawaita wateja waje tu ulinzi upo, Geita ni amani kazi zinaendelea”.
Kuelekea Jukwaa la Fursa za
Biashara Mkoani Geita, watanzania na wageni mnaalikwa kushiriki jukwaa hilo
litakalofanyika kuanzia tahere 15-16.08.2018 linaloratibiwa na Kampuni ya
Magazeti ya Serikali (TSN) kwa kushirikiana na MKoa wa Geita ambapo mtaweza
kushuhudia bidhaa zinazozalishwa Mkoani Geita lakini pia Maonesho Makubwa ya
Teknolojia ya Dhahabu yatakayofanyika kuanzia tarehe 24-29 Mwezi Septemba, 2018.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.