Bw. Ally M. Koyya, (kulia), kutoka idara ya Masoko TANESCO, akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea kwenye banda la Shirika hilo kwenye maonesho ya Nishati Mbadala yanayokwenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Juni 4, 2018.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA
la Umeme Nchini (TANESCO) limesema hakuna sababu yoyote kwa wananchi kuogopa
kutumia nishati ya umeme kwa matumizi mbalimbali ya nyumbani kwani ni nafuu mno
ukilinganisha na nishati nyingine.
Afisa
Mazingira wa Shirika hilo, Bw.Yusuf Kamote, amesema hayo kwenye maonesho ya
Nishati mbadala ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani yanayoendelea
kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Juni 4, 2018, ambapo
kauli mbiu ya mwaka huu ni “Mkaa ni ghali
tutumie Nishati mbadala”.
“Siku
zote tunasema umeme wa TANESCO ni umeme wa bei nafuu, jambo la msingi ambalo
wananchi wanapaswa kuelewa ni matumizi sahihi ya vifaa vya umeme kulingana na
mahitaji.” Alisema.
Alisema
kwa mfano mtu anatumia kifaa kinachohitaji WATI
100 (100watts) kwa saa moja lakini anatumia kifaa cha WATI 200 (200Watts) kwa saa na kwa mahitaji yanayofanana, bila
shaka hayo sio matumizi bora ya umeme.
Bw.
Kamote pia alishauri, wananchi wanapotaka kununua vifaa vya umeme, wanapaswa
kukague kiasi cha umeme kinachohitajika kwenye kifaa husika anachotaka kununua na
vifaa hivyo hupimwa kwa kutumia WATI
(Watt ).
“Ukitumia
pasi ya umeme ya WATI 1000
(1000Watts), kwa saa moja ni sawa na kutumia Unit 1 ya umeme kwa hivyo hakuna
sababu ya kununua pasi ya umeme ya WATI2000
(2000Watts), kwa matumizi ya kawaida kwani pasi ya aina hiyo kwa matumizi
sawa na ile ya WATI1000, matumizi yake yataongezeka, kutoka unit 1 hadi uniti 2.”
Alifafannua.
Akieleza
zaidi Bw. Kamote hakuna sababu tena ya kutumia mkaa kama nishati ya kupikia
kwani hivi sasa yapo majiko ya umeme ambayo yanasaidia kudhibiti matumizi
yaumeme yasiyo sahihi kwani.
“Kinachohitajika
mpishi unatakiwa kuandaa vyakula unavyotaka kupika kabla ya kuwasha jiko lako
la umeme, vyakula vikiwa tayari hapo ndipo unatakiwa kuwasha jiko lako tayari
kwa kupika.” Alisema na kuongeza
Maonesho
hayoyakliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, yalizinduliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wiki
iliyopita na yanatariwa kufungwa na Rais John Magufuli, Jumanne Juni 5, 2018.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Kanosa ya jijini Dar es Salaam, wakipatiwa maelezo ya kitaalamu na wataalamu wa TANESCO (Kushoto).
Afisa Mazingira wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Bw. Yusuf Kamote, (kulia), akimsikiliza Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Bi. Samia Chande. |
Wanafunzi wa shule ya sekondari Kanosa ya jijini Dar es Salaam, wakipatiwa maelezo ya kitaalamu kuhusu matumizi bora ya nishati ya umeme walipotembelea banda la Shirika hilo leo Juni 4, 2018.
Bw. Ally M. Koyya, (kulia), kutoka idara ya Masoko TANESCO, akimsikiliza mwananchi huyu aliyefika kwenye banda la Shirika hilo kupata elimu ya umeme.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.