ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 4, 2018

YAYA TOURE AMCHANA PEP GUARDIOLA.


Aliyewahi kuwa kiungo wa Manchester City, Yaya Toure, amemchana kocha Pep Guardiola akisema ana ubaguzi kwa baadhi ya wachezaji haswa wa Afrika.
Toure ambaye ameondoka Manchester City mwezi Mei 2018 ikiwa ni baada ya kukaa kwa muda wa miaka minane ndani ya timu hiyo, amefunguka na kueleza hayo kufuatia kutokuwa na maelewano mazuri baina yake na Guardiola.

Kiungo huyo ambaye amefanya vizuri na kikosi hicho huku akichukuwa ubingwa mara mbili wa Ligi Kuu England, ameeleza kuwa Guardiola amekuwa na ubaguzi kwake tangu akiwa FC. Barcelona.

Nyota huyo kutoka Ivory Coast, amefunguka na kueleza mengi huku akisema Guardiola atakuwa ana tatizo na wachezaji wa kiafrika kutokana na vitendo vya ubaguzi ambavyo amekuwa akivionyesha kwao.

Aidha, mchezaji huyo ameeleza si mara ya kwanza kuyasema hayo bali hata wakati akiwa Barcelona matukio kama hayo ya kutengwa na kocha huyo yalikuwa yakifanyika kwake huku akisema inawezekana alikuwa akimuonea wivu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.