ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 4, 2018

VIDEO:- SIMBA YATIMBA NUSU FAINALI YAIBANJUA K. SHARKS KWA MATUTA 2-3 SPORTS PESA SUPER CUPGSENGOtV
MABINGWA wa Tanzania Bara, Simba SC wamefanikiwa kusonga mbele  katika mchezo wake wa kwanza wa SportPesa Super Cup uliochezwa jioni hii na kumalizika hivi punde katika Uwanja wa wa Nafraha mjini Nakuru, Kenya baada ya kuigagadua Kariobangi Sharks kwa njia ya penati 2-3.

Jonas Mkude ndiye aliyepiga penati ya mwisho kwa Simba, akifunga kiufundi bila kutumia nguvu kubwa zaidi ya akili na ujanja kumwamisha golikipa wa Shark.

Katika michuano hiyo timu nyingi zimeonekana kuwatumia wachezaji wake wapya zilizowasajili Kwa Simba miongoni kwa waliosajiliwa ni mshambuliaji kutoka Tanzania Prisons, Mohammed Abdallah na Singida United na mpachika mabao kutoka Mbao FC, Habib Kiyombo.

Mchezo wa pili na wa mwisho wa hatua za awali kati ya wenyeji wengine, AFC Leopards dhidi ya Singida United utakaoputwa kesho.

Singida itakwenda Uwanja wa Nafraha hiyo kesho baada ya kuwashuhudia ndugu zake, Yanga na JKU kutoka Tanzania pia wakitupwa nje ya mashindano na timu za Kenya, huku Simba ikijitutumua na kusonga mbele kuipeperusha pendera ya Tanzania kwenye michuano hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.