ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 5, 2018

MAZISHI YA MAPACHA WALIOUNGANA MARIA NA CONSOLATA MWAKIKUTI KUFANYIKA KESHO JUMATANO MKOANI IRINGA

IRINGA
MAZISHI ya Mapacha walioungana MARIA na CONSOLATA MWAKIKUTI yamepangwa kufanyika Mkoani Iringa siku ya Jumatano tarehe 6 mwezi huu katika Makaburi ya kanisa catholic Tosamaganga Wilayani Iringa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoani Iringa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. RICHARD KASESELA amesema katika kikao walichokaa hii JANA Jumatatu na wanafamilia wamekubaliana, Mazishi kufanyika siku ya Jumatano katika eneo la Tosamaganga. 

Insert…………….. RI

KASESELA amesema mazishi hayo yatahudhuriwa na viongozi wengi wakubwa wa Kitaifa hivyo amewaomba wananchi watakaopata nafasi kujitokeza kuwaaga mapacha hao.

Insert……………….. TUNTUFYE 

Kwa upande wake Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani katika Hospitali ya Rufaa Mkoani Iringa Dr. FAITH KUNDI amesema kuwa aliwapokea Maria na Consolata tarehe 17/05/2018 wakitokea Hospitali ya Muhimbili huku tatizo kubwa lilionekana kwa Maria ambaye alikuwa ana tatizo la upumuaji.

Insert……………... CLIP 3 DR FAITH KUNDI

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.